31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Zahera aanika siri ya chapa chapa ya Yanga

 NA MOHAMED KASSARA, DAR ES SALAAM


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema anaamini moyo wa kujitolea walionao wachezaji wake utakifanya kikosi chake kuendelea kupata matokeo mazuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Zahera ametoa kauli hiyo, akitoka  kukiongoza  kikosi chake kuiabuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania na kukalia kiti cha uongozi wa Ligi Kuu, baada ya kufikisha pointi 35, huku akiiteremsha Azam FC yenye pointi 33 katika nafasi ya  pili, Simba iliyo na pointi 27 katika nafasi ya  tatu.

Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu, Yanga imeshinda michezo 11 na kutoka sare mbili, baada ya kushuka dimbani mara 13.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Zahera alisema moyo wa kujituma wa vijana wake ndiyo silaha yao kuu iliyokifanya kikosi chake kutopoteza mchezo hadi sasa na kudai kuwa anaamini wanaendelea na kasi yao hiyo.

“Nashukuru kupata wachezaji wenye moyo wa kujitolea kwa ajili ya timu, kikosi changu si ghali kama walivyo washindani wetu, tunachowashangaza tunaweza kupata matokeo mazuri katika michezo yetu, licha ya kukabiliwa na matatizo mbalimbali, ikiwemo mishahara.

“Kama nilivyosema awali wakati mwingine tunapitia magumu, lakini wachezaji wangu wamekuwa hawaniangushi, wanapoingia uwanjani fikra zao ni kupata matokeo mazuri, mengine yote wanaweka kando, tumekuwa tukiwakosa baadhi ya wachezaji katika michezo yetu kadhaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini atakayepewa nafasi anaonyesha juhudi, naamini tutaendelea kufanya vizuri,” alisema Zahera, mwenye uraia wa DRC na Ufaransa.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, Zahera alitamba kuwa kikosi chake kitaondoka na pointi zote tatu, mchezo huo na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi.

“Tumejiandaa vizuri kwa mchezo huo, niliambiwa timu haikupata pointi hapa msimu uliopita, najua ugumu wa kucheza hapa, vijana wangu wapo katika morali ya juu sana, wanatambua umuhimu wa kukaa kileleni, hivyo tunaomba Wanayanga wasiwe na hofu, tutahakikisha tunashinda na kurudi na pointi  tatu muhimu, alisema kocha huyo msaidizi wa timu ya Taifa ya Jamhuri wa Kidemokrasia Kongo (DRC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles