31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Zahanati zamchefua Jafo, akatisha ziara

Florence Sanawa -Mtwara

WAZIRI wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amelazimika kukatisha ziara yake mkoani Mtwara, baada ya kutoridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Miradi hiyo, ni pamoja ujenzi wa vituo vya afya kususua hali inayosabaisha  wananchi kuchelewa kupata huduma za afya.

Alitembelea wilayani Nanyumbu,Masasi na kulazimika kukatisha ziara yake wilayani Mtwara,baada ya kukagua mradi wa soko  la  kisasa na kituo cha afya cha Likombe kwenye manispaa hiyo, ambapo ameridhishwa na ujenzi huo na kulazimika kutoa agizo  kwa watendaji mkoani humo kuwa,  hadi kufikia Januari 15, mwakani kituo hicho kianze kutoa huduma

Akizungumza alipotembelea kituo cha afya cha Kilambo wilayani Mtwara  kinachosuasua kwa ujenzi, alisema hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwakuwa haimaliziki kwa wakati katika wilaya za Mtwara, Nanyumbu na Masasi.

Alisema miradi hiyo, inayotekelezwa mkoani humo imekuwa haiendi vizuri hali ambayo  inachelewesha wananchi kupata huduma hiyo kama vile inavyotarajiwa na kupelekea wananchi kupata usumbufu wa kufata matibabu mbali, wakiwamo akina mama wajawazito.

Alisema  fedha hizo, zilipokelewa mwishoni  mwa mwaka 2017/18,kusababisha kuvuka kwa mwaka wa fedha hali iliyosababisha miradi kuchelewa kuanza ambapo katika kituo cha afya Kilambo, ulitakiwa kukamilika Aprili mwaka huu.

“Huu mkoa unanini mbona hamna usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo miradi ya afya yote mibovu yaani, unakuta mafremu bado hamjaweka masinki bado mmeona mimi nakuja hapa ndiyo mnaweka mafundi kuanza kuchimba chimba udongo wakati siku zote hakuna kinachoendelea, nimetembelea Nanyumbu mpaka Masasi, miradi  haijatekelezeka naomba niseme mkoa wa Mtwara wote una matatizo”

“Rais ametoa fedha nyingi mwaka jana kwa ajili ya miradi ya afya, mnaleta mchezo mchezo alafu mmesikia nakuja mnaanza kunifanyia maigizo, mjue mnawaumiza wananchi wenu ambao walipaswa kutumia huduma hii.

“Unajua miradi ya afya, inatelekezwa nchi nzima maeneo mbalimbali imefanyika vizuri, mkoa huo utekelezaji wake umekuwa siyo mzuri, lazima hatua zichukuliwe,” alisema Jafo

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Henry Nyanzi alisema walipokea Sh milioni 500 ajili ya ujenzi huo,hadi wametumia Sh milioni 400.

Kuhusu changamoto, alisema ni pamoja na mvua zinazoendelea kunyesha  maeneo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles