24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Zabuni za mafuta nchini kugawanywa kuongeza ufanisi

Uwagizaji wa pamoja hupunguza idadi ya Meli za Mafuta zinazokuja nchini.
Uwagizaji wa pamoja hupunguza idadi ya Meli za Mafuta zinazokuja nchini.

Na Justin Damian,

Katika kipindi cha kuanzia Januari, 2015 bei ya Mafutakatika Soko la Dunia ziliendelea kushuka na kufikia wastani wa Dola za Marekani 38 kwa pipa la Mafuta Ghafi kwa Mwezi Disemba mwaka huo.

Aidha, wastani wa bei ya mafuta yaliyosafishwa kwa kipindi cha kati ya mwezi Januari na Desemba, 2015 ulikuwa kama ifuatavyo: Petroli kutoka Dolaza Marekani 669 hadi Dola za Marekani 437 kwa tani; Dizeli kutoka Dola za Marekani 570 hadi Dola za Marekani 335 kwa tani; na Mafuta ya Taa/Ndege kutoka Dola za Marekani 570 hadi Dola za Marekani 363 kwa tani ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 35 kwa Petroli,asilimia 41 kwa dizeli na asilimia 39 kwa Mafuta ya Taa/Ndege, sawia.

Bei ya Mafuta katika Soko la Ndani hutegemea bei ya mafuta ya petrol katika Soko la Dunia pamoja na Thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na Dola ya Marekani.

Katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2015 wastani wa bei za mafuta katika Soko la Ndani kwa lita ilikuwa: Petroli Shilingi 1,973, Dizeli Shilingi 1,808 na Mafuta ya Taa Shilingi 1,739 ikilinganishwa na wastani Shilingi 2,186 kwa Petroli, Shilingi 2,082 kwa Dizeli na Shilingi 2,030 kwa Mafuta ya Taa kwa kipindi kama hicho katika Mwaka 2014.

Ili kurahisha uigizaji wa mafuta na kutoa unafuu kwa mlaji wa mwisho Serikali iliaanzisha Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency – PBPA) mwezi Januari, 2016.

Wakala huo pamoja na kazi nyingine unatekeleza majukumu yailiyo kuwa Kampuni Binafsi ya kuratibu Uagizaji wa Mafuta ya Petroli kwa Pamoja (Petroleum Importation Coordinator Limited – PICL).

Kampuni hiyo ili kuwa inamilikiwa na Kampuni binafsi za uagizaji na usambazaji wa mafuta ya petrol nchini.

Pamoja na faida nyingine kwa mujibu wa Wizara ya Nishati na Madini lengo la kuanzisha Wakala huu n ikuongeza ufanisi katika shughuli za uagizaji mafuta ya petrol nchini.

Miongoni mwa majukumu ya Wakala huu ni kusimamia Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta ya Petroli kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement System – BPS) na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya petrol ya kutosha wakati wote nchini.

Katika Mwaka 2016/17, Wakala utaanza pia kuratibu uagizaji wa Liquefied Petroleum Gas – LPG pamoja na mafuta mazito(Heavy Fuel Oil – HFO) kupitia mfumo wa BPS.

Mfumo wa kuagiza mafuta kwa pamoja ulianza tangu mwaka 2011 lakini chini ya PBPA kama mamlaka inayoshughulika na suala hili ulianza mwezi Februari mwaka jana.

Hata hivyo,makampuni machache ya mekuwa ya kifikia kwenye hatua ya mwisho ya kuomba zabuni ya kuagiza mafuta jambo ambalo linaonyesha ushindani bado simzuri kama ambavyo ingetarajiwa.

Kwa mfano, katika zabuni ya mwezi wa kumi makampuni yaliyoweza kupita kwenye mchujo wa awali yalikuwa ni makampuni 30 na yaliyofanikiwa kuingia kwenye hatua ya mwisho kabisa ya zabunini makampuni manne tu.

Alipoulizwa ni kwanini makampuni machache yamekuwa ya kiingia kwenye mchujo wa mwisho, MenejaUgavi wa PBPA Raymond Luseko alisema PBPA wamefanya tathmini na kugundua sababu mbalimbali ikiwamo ushindani mkubwa ulioko kwenye bei za uletaji wa mafuta.

“Kwa mfano kampuni ya iliyoshinda mwezi Octoba imekuwa ikishiriki kuomba zabuni tangu mwaka 2012 na leo ndiyo wamebahatika kupata,” anaeleza

Luseko anasema kuwa pia kumekuwa hoja na mawazo kuwa thamani ya zabuni imekuwa ni kubwa sana jambo ambalo kampuni nyingi zimeshindwa kushiriki kutokana na kuhitajika kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Kwa mujibu wa meneja huyo, PBPA imeamua kugawanya tenda ambayo ilikuwa ikitolewa kwa kampuni moja. Aliliambia gazeti hili kuwa kuanzia mwezi Novemba zabuni itagawanywa katika sehemu ndogondogo ilikuyawezesha makampuni mengi zaidi kushiriki kuomba kuagiza mafuta.

Wazohilinijemakwakuwakamazabuniitagawanywakatikasehemundogondogoniwazikuwamakampunimengizaidiyatashirikinahivyokuletaushindaniambaoutasababishabeizamafutakushukanakumfikiamlajiwamwisho.

Mafuta ni hitaji muhimu kwa nchi na kupanda kwake huathiri bei ya karibu kila bidhaa. Utaratibu huu mpya wakugawanywa kwa zabunini hatua muhimu ambayo ni matarajio ya wengi kuwa utaweza kuvuta makampuni makubwa na ya katika kushindania zabuni na hivyo kufanya bei zishuke jambo ambalo ni faraja kwa walaji wa mwisho na wananchi kwa ujumla.

Jambo muhimu ni kwa PBPA kuhakikisha inasimamia sheria na kutoa zabuni bila ya upendeleo.

Biashara ya mafuta na haswa uagizaji wake hufanywa na makampuni yenye uwezo kubwa na yanaweza kutumia uwezo wake wa kifedha kufanya ushawishi jambo ambalo liwaumiza wananchi wengi .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles