TAMASHA la burudani linalohusisha wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali linaloitwa After School Bash linafanyika leo kwenye ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam ambapo nyota mbalimbali wa muziki wakiongozwa na David Genzi ‘Young Dee’ watatumbuiza.
Akipiga stori na Swaggaz kuhusiana na tamasha hilo, Young Dee alisema amejiandaa vya kutosha kuhakikisha
mashabiki wake watakaokwenda kwenye ufukwe huo watapata burudani ya nguvu kutoka kwake.
“Binafsi nimejiandaa poa kuhakikisha kwamba natoa burudani ya kutosha kwa mashabiki wangu, kikubwa watu wote wajitokeze kwa wingi.
Hili ni tamasha la mwisho kwa mwaka huu hivyo lazima tule bata vya kutosha,” alisema Young Dee.
Mbali na Young Dee jukwaa la After School Bash mwaka huu litashambuliwa na nyota wengine kama Jux, Vanessa Mdee, Ruby, Weusi, Stamina, Young Killer, Chemical na Izzo Biznes na wengine wengi.