YJ ampa makavu Niva

0
791

Christopher Msekena

MSANII wa Bongo Fleva, Yakuti Ramadhan ‘YJ’, amekanusha vikali tuhuma za mwigizaji, Niva Super Mariyoo, kuhusika katika uandishi wa ngoma yake, Achia aliyomshirikisha Billnas na Mr T Touch.

Akizungumza na MTANZANIA jana, JY  ambaye ni mtoto wa Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhan, alisema madai hayo siyo ya kweli ni kitendo cha Niva kusema hivyo ni kumvunjia heshima sababu ameshamsaidia mambo mengi.

“Niva alidai kuwa ameandika vesi ya Billnas kwenye ngoma yangu jambo ambalo siyo la kweli, amenivunjia heshima sababu hajahusika na lolote kwenye ile ngoma,” alisema YJ ambaye sasa anatamba na wimbo Achia Remix aliowahirikisha Nay wa mitego na Stamina.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here