28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yazindua kadi mpya za uanachama Bungeni

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KLABU ya Yanga Sc imefanya uzinduzi wa kadi mpya za uanachama za Kieletroniki kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiitaka klabu hiyo kuweka mipango ya kutafuta wachezaji wenye vipaji kutoka katika ligi ndogo ndogo na wale wanaotoka mitaani.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson.

Uzinduzi wa kadi za kieletroniki ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko ya kidigital na mfumo wa uendeshaji wa klabu kwa mujibu wa katiba ya Yanga toleo la 2021.

Akizungumza leo Februari 18,2022 wakati wa uzinduzi huo,uliohudhuriwa na wanachama wabunge wa timu hiyo,wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa timu hiyo ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais Ikulu Kazi Maalum George Mkuchika Spika Tulia amesema kuna haja ya Klabu hiyo kuvisaidia vipaji ambavyo vipo mitaani.

Amesema anatamani kuona  wachezaji kutoka katika Ligi ndogondogo wanapewa nafasi ya kuzichezea Klabu kubwa huku akiwataka viongozi kutuma wawakilishi wakati zikichezwa ligi ili waweze kupata wachezaji wazuri.

“Kwahiyo mimi natamani viongozi katika hatua zile ambazo mnaendelea nazo basi muweke mipango mahususi kwa ajili ya hizi ligi ndogo ndogo zinazokuwa maeneo mbalimbali au hizi Cup ndogo ndogo mkisia Cup mahali basi mtume hata mwakilishi saa zingine si kocha,kocha ni mtu mkubwa.

“Wale watu wenu kule mikoani hii si timu ya Wananchi mpo kila mahali wawe wanahudhuria maeneo ili wale wachezaji wadogo wanaocheza kule waweze kuonekana na waje katika Klabu kubwa kama hii na inaweza kuwachukua na kuanza kuwalea kwa sababu tunatamani na sisi tuwe na majina makubwa makubwa.

“Kama hayo ambayo tunayasikia kwingine na hatutaweza kupata hayo majina makubwa kama Klabu kama Yanga haitawatafuta hao vijana na kaunza kuwalea  na wapo wale wanaohitaji  kulelewa kidogo tu na tutawapata kule mtaani,”amesema Dk. Tulia.

Pia, Spika Tulia ameitaka timu hiyo kukekemea kwa nguvu zote vurugu michezoni ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya mashabiki ambao huwa wanaingia viwanjani kwani michezo ni furaha na undugu.

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa timu hiyo, Dominick Albinus amesema tukio hilo ni mwanzo wa wanawachama waliojiandikisha kuanza kupata kadi zao ambapo ndani ya wiki mbili wanachama wengine wataanza kupata kadi zao katika matawi yao.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Bungeni, Seif Gulamali ambaye ni Mbunge wa Manonga amesema zaidi ya wabunge 120 ambao ni wanachama wa yanga wamejisajili kupata kadi hizo wakiwemo baadhi ya Mawaziri na Naibu Waziri

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles