26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga ‘yawapa’ fedha wachezaji Coastal

5NA AMINA OMARI, TANGA

WACHEZAJI wa Klabu ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, juzi walikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 2 kutoka kwa mfadhili wa timu hiyo, Alhaji Salim Bajaber ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda cha Unga cha Pembe Tanga, ikiwa kama motisha ya timu hiyo baada ya kuifunga Yanga.
Fedha hizo zilikabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Salim Amiri kwa Nahodha wa Coastal Union, Hamis Mbwana ‘Kibacha’ mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyokuwa yakifanyika kwenye Uwanja wa Shule ya
Sekondari Popatlaly.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Makamu Mwenyekiti huyo kwanza alitumia nafasi hiyo kumshukuru mfadhili huyo, pia akiwataka wachezaji kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo wanapokuwa
uwanjani ili kuendeleza ushindi mechi zijazo.

“Jamani mnaona namna tunavyoweza kucheza vizuri na kupata ushindi, ndivyo wafadhili wetu wanafurahi lakini pia itatusaidia kujenga heshima ya timu yetu ya miaka ya nyuma, hivyo naomba tuendelee kupambana ili kuhakikisha tunamaliza ligi tukiwa nafasi tatu za juu,” alisema Salim.

Hata hivyo, alisema kuwa uongozi umeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michezo yao inayofuata, baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Ally Jangalu, kufanya kazi kubwa ya
kukinoa kikosi hicho.

Coastal Union ambao Jumamosi iliyopita walifanikiwa kuifunga Yanga katika mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania bara mabao 2-0, wapo kwenye maandalizi ya mwisho wakijiandaa na mechi yao dhidi ya Ndanda FC itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Kwa upande wake, nahodha wa timu hiyo, Kibacha aliahidi kushirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo, ili kuweza kurudisha furaha kwa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo.

“Niseme tu sisi kama wachezaji tumefarijika sana na kuona namna tunavyojaliwa na kuthaminiwa, hivyo ni wajibu wetu nasi kutimiza wajibu kwa kuweka jitihada ili ushindi uweze kupatikana kila mchezo,” alisema Kibacha.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles