Yanga yawaonya mashabiki wao

0
1004
Mashabiki wa Yanga, wakiwa wamebeba mfano wa jeneza lenye kitambaa cha rangi ya watani wao Simba, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba na Yanga, uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.

Na TIMA SIKILO –DAR ES SALAAM

VIONGOZI wa Yanga wamewataka wapenzi wa soka hapa nchini kutotembea na bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mfukoni.

Yanga Jumamosi iliyopita ilitoka sare ya mabao 2-2 na mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema katika mchezo uliopita walikiangalia kikosi chao na kufahamu wana uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika ligi iwapo wataendelea kujipanga vizuri.

Alisema wapo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar lengo lao kubwa likiwa ni kujua kikosi chao cha kwanza na ni wachezaji gani ambao wanaweza kuwapa matokeo na hata kutwaa ubingwa wa Bara.

“Kwenye ligi hii watu wasitembee na bingwa mkononi, sisi tumejipanga na tunaendelea kupambana, lolote linaweza kutokea.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunakiimarisha kikosi chetu zaidi eneo la ushambuliaji na tutaleta mchezaji mwingine wa eneo hili hivi karibuni,” alisema.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanashika nafasi ya tano, wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 12.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here