25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yatua Kigoma bila Shikalo, Molinga

Na THERESIA GASPER -DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga kimewasili mkoani Kigoma jana na jumla ya wachezaji 23 kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Mgongo FC na Mbao FC, huku wakiwaacha wachezaji wao, David Molinga, Farouk Shikalo na Papy Tshishimbi.

Timu hiyo ya Yanga itazitumia mechi hizo mbili kwa lengo la kufanya maandalizi kuelekea mchezo wake wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Iringa United, pamoja na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lakini pia timu hiyo inakabiliwa na mchezo dhidi ya Watani zao, Simba, unaotarajiwa kuchezwa Januari 4 mwakani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema mechi hizo zitamsaidia kocha wa timu yao, Charles Mkwasa, kufahamu ni sehemu gani kuna kasoro kabla ya kucheza mechi inayofuata.

“Wachezaji waliokwenda Kigoma ni 23, lakini hata hivyo tuliwapa mapumziko ya wiki moja nyota wetu wa kigeni kwa ajili ya kwenda kuangalia familia.

“Hata hivyo, wengine ilishindana kwenda ambao ni Molinga, Shikalo na Tshishimbi, ambako tayari tulikuwa hatujawakatia tiketi ya kwenda na wenzao Kigoma, hivyo wamelazimika kubaki, lakini wanaweza wakaja kesho (leo) kuwafuata wenzao,” alisema.

Alisema wanaamini benchi la ufundi litatumia mechi hizo kufahamu ni wapi wataanzia katika mechi zinazowakabili mbele yao.

Hata hivyo, kuna taarifa kwamba wachezaji wa kikosi hicho walipewa mishahara yao ya miezi miwili ambayo walikuwa wakidai klabu hiyo ya Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles