28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Yanga yatinga nusu fainali FA

NA TIMA SIKILO

KIPA wa Yanga, Klaus Kindoki, alikuwa shujaa Yanga ikiifunga Alliance FC kwa penalti 4-3 mchezo wa robo fainali Kombe la FA maarufu Azam Sport Federation Cup iliyochezwa Machi 30, 2019 Uwanja CCM Kirumba jijini Mwanza.

Hadi dakika 90 zinakamilika, timu zote zilikuwa zimefungana bao 1-1 huku Yanga wakitangulia dakika ya 33 kupitia kwa Heritier Makambo kabla ya Jacob James kuisawazishia Alliance FC dakika ya 62.

Katika mikwaju ya penalti, Kindoki alipangua kiki ya Martin Kiggi na nahodha Siraji Juma huku Dickson Ambundo akipiga nje. Waliopata penalti zao upande wa Alliance ni Joseph James, Godfrey Luseke na Samir Vincent.

Waliofunga penalti za Yanga ni Paul Godfrey, Thaban Kamusoko, Haruna Moshi na Deus Kaseke wakati Kelvin Yondani na Mrisho Ngassa wakikosa.

Katika mchezo huo wa robo fainali uliochezeshwa na Florentina Zablon, timu zote mbili zilionyesha kandanda nzuri huku zikishambuliana kwa zamu.

Kutokana na matokeo hayo, Yanga wanajiandaa kwenda mkoani Iringa kuwakabili Lipuli FC, mchezo wa nusu fainali utakaochezwa Uwanja wa Samora na timu itakayoshinda itatinga fainali na kusubiri kucheza na mshindi kati ya Azam FC na KMC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles