23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga yapiga hesabu kali

DSC_0802

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, timu ya Yanga, leo itakuwa kibaruani katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuivaa Mo Bejaia ya Algeria.

Yanga bado inapambana hadi sasa ili kuhakikisha inatinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga Mo Bejaia na baadaye iifunge TP Mazembe ya DR Congo ili iweze kusonga mbele.

Mazembe ambao ni mabingwa wa Afrika mara 5, kesho nao watakuwa wakiivaa Medeama na dua za Yanga ni kuona Wacongo hao wakipata ushindi.

Yanga kama mambo yatakuwa mazuri leo kwa kuifunga Bejaia watafikisha pointi nne huku ikiomba Mazembe iifunge Medeama kwao.

Yanga inahitaji kuchanga karata zake vema ili iifunge Bejaia leo na baadaye waifunge Mazembe ili wawe washindi wa pili kwa kufikisha pointi saba na wakiomba dua ili Mo Bejaia na Medeama watoke sare katika mchezo wa mwisho katika Kundi A.

Kama hesabu hizo zitakwenda sawa, TP Mazembe itakuwa ikiongoza Kundi  A kwa kufikisha pointi 13 huku Yanga  ikiwa ya pili na pointi saba wakati Mo Bejaia na Medeama wakifuatia kila mmoja akiwa na pointi sita.

Kwa hesabu hizo TP Mazembe na Yanga zitakuwa zimetinga nusu fainali hivyo kuungana na timu nyingine za Kundi B katika michuano hiyo.

Yanga imepanga kuhakikisha hesabu hizi zinatimia ambapo jana walifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Gymkhana kuhakikisha wanaifunga Bejaia.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van de Pliujm, amesema kuwa kikosi chake kinaingia uwanjani kikiwa kinasaka pointi tatu ambazo zitawafanya wawe na uhakika wa kusonga mbele.

“Nimekiandaa kikosi changu kwanza kwa kuwaondoa dhana ya kuwa tumeshapoteza nafasi ya kuingia nusu fainali, lakini pia nimegawa majukumu kwa kila mchezaji atakayeingia uwanjani ahakikishe tunapata ushindi wa pointi tatu muhimu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles