26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA YAPEWA MCHOVU, SIMBA KAZI SI RAHISI

Zainab Iddy -Dar es salaam

DROO ya michuano ya Kombe la Shirikisho maarufu Kombe la Azam, ikiwa hatua ya 64 bora, imechezeshwa jana, ambapo Yanga imepangwa kuumana na Iringa United, Simba itakipiga na Arusha FC, huku Azam ikipewa African Lyon.

Yanga ambao ni mabingwa wa kwanza wa taji hilo ilipolitwaa msimu wa 2015-16 , itamenyana na Iringa United ambayo inaburuza mkia katika msimamo wa Kundi A wa Ligi Daraja la Kwanza.

Msimu uliopita, Wanajangwani hao waliishia hatua ya nusu fainali,  baada ya kuondolewa na Lipuli  kwa mabao 2-0.

Kwa upande wa mahasimu wao Simba, ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu wa 2016/17, itapimana ubavu na Arusha  inayokamata nafasi ya nne katika msimamo wa Kundi B wa Ligi Daraja la Kwanza.

Msimu uliopita, Simba iliondolewa na Mashujaa FC, baada ya kuchapwa mabao 3-2.

Azam kwa upande wake itatoana jasho na African Lyon ambayo inashika nafasi ya pili, katika msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza.  

Kulingana na matokeo ya droo hiyo, timu nyingine ni  Mbuni ambayo itakipiga na KMC, Alliance Vs Transit Camp , mechi itachezwa Uwanja wa Nyamagana, wakati Ndanda wataialika Cosmopolitan dimba la Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Jeshi Worriers  wataumana na Dodoma FC  Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, Majimaji  watashindana na  Pamba, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Area C Vs Panama FC, Gwambina Vs Mbeya Kwanza, Geita Gold Vs Pan African, Sahare All Stars Vs Njombe Mji, wakati Rufiji United watasafiri hadi Kagera kuumana na Kagera Sugar.

Timu nyingini ni Coastal Union Vs African Sports, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Namungo Vs Green Warriors, Uwanja wa Majaliwa Complex,  JKT Tanzania Vs Boma FC dimba la Meja Generali Michael Isamuhyo, Dar es Salaam.

 Lipuli Vs Dar City, Tanzania Prisons  Vs Mlale FC, Uwanja Sokoine Mbeya, Mtibwa Sugar Vs Rhino Rangers,  dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.

Milambo FC Vs Ruvu Shooting, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, Mbao FC Vs Stand United, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza,  wakati Nyamongo FC watakuwa wageni wa Biashara United, Uwanja wa Karume, Musoma.

Nayo Mawenzi FC  itaialika Mtwivila City,  Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Kitayosa FC itasafiri hadi mkoani Dodoma kucheza na Mpwapwa United, Friends  Rangers itatua Kigoma kukipiga na Talinega FC, dimba la Lake Tanganyika, Kigoma.

Kasulu Redstars itaumana na Ihefu FC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Toto African Vsa Gipco, Uwanja wa CCM Kirumba wakati The Might Elephant  itachanga karata zake kwa kutunishiana msuli na Mashujaa FC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles