24.6 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yapewa masharti kumnasa Tchetche

Kipre Tchetche
Kipre Tchetche

Na ADAM MKWEPU -DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Azam FC, umesema upo tayari kufanya mazungumzo na Yanga wanaodaiwa kuwania saini ya mshambuliaji wao, Kipre Tchetche, ili kuimarisha kikosi chao.

Azam imefikia hatua hiyo baada ya kuwepo kwa madai kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wametuma ‘mashushushu’ nchini Ivory Coast ili kumshawishi nyota huyo ajiunge na timu hiyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana Mkurugenzi Mtendaji wa Azam FC, Saad Kawemba, alisema hawana presha juu ya kitendo kinachofanywa na Yanga ikiwa watafuata utaratibu wa usajili.

“Ujanja wanaofanya Yanga hauwezi kuwasaidia kwani Tchetche bado ana mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Azam, hivyo hata kama  wakimfuata na kufanya naye mazungumzo ni  lazima waje kumalizana na uongozi.

“Tupo tayari kufanya biashara na Yanga, tunajiamini na tunaamini tunaweza kuzungumza na klabu yeyote ambayo itaonyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili Tchetche,” alisema.

Aidha, Kawemba alisema klabu hiyo ina mpango wa kukifanya kituo chao cha kukuza vipaji kuwa miongoni mwa vituo bora barani Afrika ili kiweze kufanya biashara ya kutengeneza na kuwauza wachezaji wenye vipaji.

“Azam tunataka tubadilike kwa kila kitu ndani ya miaka minne ijayo, hasa katika mpango wa kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi na kuwauza, hivyo suala la Tchetche halitunyimi usingizi, Yanga waje kwa mazungumzo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles