23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga yamtema rasmi Telela

Salum Telela
Salum Telela

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Yanga, umethibitisha rasmi kumtema kiungo wake, Salum Telela, hivyo kuacha milango wazi kwa klabu yoyote itakayomhitaji.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kiungo huyo kudaiwa kusaini mkataba na klabu ya Simba, jambo lililokanushwa na kiungo huyo ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa tayari mchezaji huyo ameingia mkataba wa miaka miwili na Simba, hata hivyo Telela mwenyewe amekanusha na kudai kuwa hajazungumza na timu yoyote.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, alisema milango iko wazi kwa timu yoyote inayomtaka kwani wao wameshamalizana naye.

“Taarifa mbalimbali zilikuwa zimezagaa katika vyombo vya habari kuwa tumemalizana na Telela, lakini tulikuwa hatujathibitisha, sasa nathibitisha rasmi kuwa sisi na Telela basi, ni mchezaji huru anayemtaka milango iko wazi,” alisema Muro.

Hata hivyo, taarifa za ndani kutoka katika klabu hiyo zinadai kuwa licha ya Telela mkataba wake kumalizika, kiungo huyo hakuweza kuendelea kuwa na timu kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri na kocha mkuu wa kikosi hicho, Hans Van der Pluijm.

“Telela amekuwa akimuonyesha kocha dharau za wazi kabisa kama akiwa hajapangwa kwenye kikosi cha kwanza, hivyo kwa tabia hiyo uongozi umeona usiendelee kubaki na mchezaji ambaye hana nidhamu,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho pia kiliendelea kusema kuwa Telela ni mchezaji mzuri lakini nidhamu yake ambayo alikuwa akiionesha kwa kocha ndiyo iliyomfanya ashindwe kuendelea kuwepo kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles