24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yakwea kileleni

2NA OSCAR ASSENGA, TANGA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamekwea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada ya kuifunga bao 1-0 timu ya African Sports katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bao hilo lilifungwa katika dakika 90 ya mchezo huo kupitia kwa Thabani Kamusoko, baada ya kupokea pasi ya Donald Ngoma hivyo kuifanya Yanga kushika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 27 huku Azam FC wakishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 26.

Yanga walianza mchezo huo kwa kasi ambapo katika dakika ya 22 walikosa bao la wazi kupitia kwa mshambuliaji wake, Simon Msuva, baada ya kushindwa kuunganisha krosi ya Ngoma.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Suleiman Kinugani kutoka Morogoro, African Sports walifanya mabadiliko katika dakika ya 37 kwa kumtoa Mohamed Issa na kuingia James Mendy.

Mchezo huo uliendelea ambapo katika dakika ya 41 mwamuzi wa mchezo huo alimwonyesha kadi ya njano kipa wa African Sports, Zakaria Mwaluko, kutokana na kuchelewesha mpira na hivyo timu hizo kwenda mapumziko bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mashambulizi ambapo katika dakika ya 55 mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke, alikosa bao baada ya kupiga shuti na kuokolewa na beki wa African Sports, Mwaita Gereza.

Katika dakika ya 68 mshambuliaji wa Sports, Pera Ramadhan, alianguka chini na hivyo kusimama kwa muda baada ya kuumia wakati akipiga mpira huo.

Katika dakika ya 75, Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Amissi Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Malimi Busungu na African Sports walimtoa Mohamed Mtindi na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Issa.

Yanga walifanya tena mabadiliko katika dakika ya 82 kwa kumtoa Kaseke na kuingia Godfrey Mwashiuya.

Hadi dakika 90 zinamalizika Yanga walitoka kifua mbele kwa ushindi huo wa bao 1-0.

 

African Sports:

Zakaria Mwaluko, Pera Ramadhan, Khalfan Twenye, Juma Shemvuni, Rahim Juma, Mussa Chambega, Hussein Issa, Mussa Kizenga, Hassan Materema, Mwaita Gereza, Mohamed Issa.

Yanga:

Deogratius Munishi, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Vicent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Deus Kaseke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles