26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yakodishwa rasmi

dsc_6180

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BODI ya wadhamini wa klabu ya Yanga imeweka hadharani mkataba wa miaka 10 wa kigogo anayetaka kuikodisha klabu hiyo, ikiwa imepita miezi miwili tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa dharura wa wanachama Agosti 6, mwaka huu.

Bodi hiyo chini ya Mjumbe Francis Kifukwe, imetengua kitendawili hicho cha muda mrefu baada ya wanachana kuridhia kwa kauli moja kumkodisha kigogo huyo aliyetaka kuchukua asilimia 75 ya mapato, huku 25 ikibaki kwa wanachama.

Baadhi ya vipengele vya mkataba wa kukodishwa timu hiyo kwa miaka 10 vinaonyesha kuwa kuanzia sasa klabu itajulikana kwa jina la Yanga Yetu Limited kutoka Yanga Africans Sports Club.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na  Baraza la Wadhamini la Yanga, ilieleza kuwa mkataba huo ulifanyika kwa kuzingatia haki miliki kutolewa kwa mkodishwaji ambapo jina lake na nembo zitatumika kibiashara na kuendesha shughuli za timu ya soka, bila  kuingiliwa kwa muda wa miaka 10 kuanzia Septemba mosi, mwaka huu.

Kipengele kingine cha mkataba huo kinaeleza  kuwa kigogo huyo atailipia Yanga deni la Sh  bilioni 11,676, inayodaiwa kama mmiliki na mkopeshaji mmoja.

Pia atailipa klabu hiyo kiasi cha Sh milioni 100 kwa mwaka, ambapo klabu itapata fursa ya kuwekeza kiwango kisichopungua asilimia 90 ili kuimarisha mtandao wa matawi yake.

Kwa upande wa uwanja, mkataba unaonyesha kuwa kigogo huyo atailipa klabu katika mwaka wa fedha wowote ule, kukiwa kuna faida ya fedha taslimu ya asilimia 25 itakayotumika kujenga uwanja wake wa soka, ikiwamo majukumu ya kifedha kujumuishwa ada za usajili zinatakiwa kuanzia tarehe ya ufanisi na majukumu mengine.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles