22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yakataa kuingiliwa kwenye uchaguzi

YangaNA ADAM MKWEPU DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga, umeigomea Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania ‘TFF’ kiaina baada ya kutoa ratiba yao ya uchaguzi, huku ukisisitiza kuwa hautaki kuingiliwa katika mchakato huo.

Ratiba mpya ya Yanga, wagombea wa nafasi zote wataanza kuchukua fomu leo na kesho na uongozi mpya kutangazwa Juni 12 mwaka huu.

Awali Kamati ya uchaguzi ya TFF iliyokuwa ikitekeleza agizo la Baraza la Michezo la Taifa ‘BMT’ la kusimamia uchaguzi huo, iliitaka wagombea katika  klabu hiyo kuanza mchakato wa uchukuaji fomu Mei 27 na uongozi mpya utatangazwa Juni 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit alisema, TFF haiwezi kuipangia utaratibu klabu hiyo.

“Hatutaki maslahi yetu yasimamiwe na watu ambao hatujuhi wana mapenzi na klabu gani, ndio maana hatutaki kuingiliwa na mtu yeyote, TFF watakuwa ni  waangalizi wa uchaguzi huo. lakini si kupanga mchakato wa uchaguzi huu,” alisema.

Katibu huyo aliongezea kuwa, Katiba itakayotumika katika uchaguzi huo ni ya mwaka 2010 ambapo wanachama wenye kadi mpya na zile za zamani, wataruhusiwa kupiga kura ili kuchagua viongozi wa klabu hiyo.

“Uchaguzi huu tunataka uwe wa amani na si kuwa mwanzo wa vurugu kwa kuwatenganisha wanachama wapya na zamani, hivyo tutahakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Naye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro alitoa angalizo kwa watu wanaojihusisha na hujuma za kukwamisha mchakato wa uchaguzi kuwa waache.

“Tunawajua wanaofanya hivyo na wakiendelea tutawataja bila kuwaonea aibu, hata kama wakiwa Serikalini, mwachama au TFF,” alisema Muro.

Wakati huohuo TFF imeeleza kuwa mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo utaendelea kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, kwa mujibu wa utaratibu uliotolewa awali.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ilisema kuwa fomu za uchaguzi huo zitaendelea kuchukuliwa katika ofisi za Makao Makuu ya TFF-Karume pia  kwenye tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz.

“TFF inafuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa mchakato na taarifa zote zitatolewa na TFF, kupitia wasemaji wake na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ambaye ni Wakili Msomi, Alloyce Komba.

“Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF, iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu,” alisema Lucas.

Pia aliongeza kuwa, Kamti imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu, ambapo Jumatatu saa 10:00 jioni utamalizika.

“Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu, wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010, inayotambulika serikalini hadi sasa,” alisema Lucas.

Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.

Lucas aliongezea kuwa fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya Mwenyekiti na Makamu, kwa wagombea wa nafasi ya Ujumbe Kamati ya utendaji fomu ni Sh 100,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles