27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yajifariji yaahidi kumaliza machungu Ligi Kuu

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BAADA ya kutolewa  mapema katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi wa  Klabu ya Yanga umewataka mashabiki wake  wasiwe wanyonge kwani  kikosi kizuri wanacho  na wana uhakika wakufanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara wakianzia mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Yanga  ambayo imeondolewa na River United ya Nigeria kutokana na  kupoteza mechi zote za nyumbani na ugenini, inatarajia  kukutana na Simba  Jumamosi hii Septemba 25, 2021 katika mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa  msimu mpya wa Ligi Kuu 2021/2022 kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mchezo  wa jana waliofungwa 1-0  na Rivers United nchini Nigeria, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikilwa amesema timu imecheza vizuri tofauti na ilivyokuwa nyummbani na wachezaji walipambana. 

Amesema  wanachoangalia kwa sasa ni majukumu yaliyopo mbele na wanaridhika kuwa wana kikosi kizuri kinachohitajikia ni muunganiko wa timu.

 “Tunajua mashabiki wameumia, hata sisi tumeumia lakini  wakati mwingine ni lazima upate machungu ili uweze kwenda mbele zaidi, uwape wachezaji muda na mwalimu.

“Kwa sasa tunaendelea na maandalizi ya mechi yetu ya ngao ya jamii, ni mchezo mkubwa kwetu, tutaendeleza pale tulipoishia. Tumepata hasara ya kuondolewa michuano ya Kimaifa lakini faida tumepata ni michezo  iliyotupa mazoezi.

“Sisi kama uongozi tunaridhika tuna kikosi kizuri na tunaondoka kifua mbele kwa sababu tumepambana, wachezaji wamejitoa. Tunajiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii, ni mchezo mkubwa kwetu,” amesema Mfikilwa.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bunguli amesema wapinzani wao walikuwa na mbinu ya kuwatoa mchezo kutokana na baadhi  ya  wachezaji kutajwa kuwa na Covid-19.

“Mechi iliyopo mbele yetu ni dhidi ya watani ya Ngao ya Jamii, tunakwenda kupambana, mashabiki wetu wasiwe wanyonge kabisa, kikosi tunacho kizuri,” amesema Bumbuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles