29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yaiwinda Madeama Dar

yanga

NA MOHAMED MHARIZO, DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, timu ya Yanga itaendelea kujifua jijini Dar es Salaam kuisubiri timu ya Medeama ya Ghana katika mchezo wao wa kundi A utakaochezwa Julai 16 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hatua ya timu hiyo inayonolewa na kocha Hans Van De Pluijm, kubaki Dar es Salaam huenda ni moja ya mipango yao ya kuhakikisha inajifua ipasavyo na kuidhibiti Medeama ili kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit, alisema hawana mpango wa kutoka nje ya Dar es Salaam na badala yake wataendelea kubaki kambini katika hoteli ya Bahari Beach hadi itakapovaana na timu ya  Medeama.

“Hapana timu iko hapahapa Dar es Salaam, ipo Bahari Beach na haitaenda Pemba, itaendelea kubaki hapo hapo hadi siku ya mechi na Medeama,” alisema Deusdedit ambaye muda huo alikuwa akiingia kikaoni kujadili mambo mbalimbali yanayoihusu  klabu hiyo.

Hadi sasa Yanga haina pointi katika katika mechi zake mbili ilizocheza na itakuwa inasaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Medeama katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na tayari imepoteza mechi dhidi ya MO Bejaia nchini Algeria Juni 19 mwaka huu baada ya kufungwa bao 1-0 na Juni 28 mwaka huu ilifungwa bao 1-0 na mabingwa mara tano barani AFRIKA TIMU YA tp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika kundi hilo la A, Mazembe wanaongoza wakiwa na pointi sita wakifuatiwa na MO Bejaia walio na pointi nne wakati Medeama wakishika nafasi ya  tatu kwa kuwa na pointi moja huku Yanga wakiburuza mkia wakiwa hawana pointi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles