23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga yaitunishia msuli Simba kuhusu Kessy

Hassan Ramadhani ‘Kessy’
Hassan Ramadhani ‘Kessy’

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Yanga umewatunishia msuli wapinzani wao wa jadi, Simba kuhusu usajili wa beki, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, ukidai kuwa mchezaji huyo walimsajili kihalali na hakuwa na mkataba na Wanamsimbazi hao.

Kauli hiyo ya Yanga inakuja zikiwa zimebaki siku chache kabla Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuamua kesi ya beki huyo anayeshtakiwa na timu yake ya zamani ya Simba kwa kuvunja mkataba.

Akizungumza na MTANZANIA jana Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit, alisema hawana presha kuhusu kesi hiyo kwa kuwa mchezaji huyo wanammiliki kihalali.

“Tunasubiri Kamati hiyo ifanye uamuzi wake siku ya Jumapili, kwani kila kitu kipo wazi tulimsajili Kessy kwa kufuata utaratibu na hakuwa na mkataba na timu yoyote.

“Kessy aliwahi kuonekana akiwa na uongozi wa Yanga mapema kabla ya kusajiliwa, rasmi tulimsajili Juni 20 na kupata kibali TFF Juni 21 mwaka huu,” alisema Deusdedit.

Deusdedit alieleza usajili huo ulifanyika baada ya beki huyo kumaliza mkataba wake Juni 15 mwaka huu na kusajiliwa akiwa mchezaji huru.

“Kila uamuzi tunaofanya lazima tuwe na uhakika nao, hivyo litakuwa jambo la kushangaza sana iwapo madai ya watani  wetu yatakuwa ya kweli na ndio maana  tumetulia tukisubiri uamuzi wa Kamati hiyo,” alisema Deusdedit.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles