23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga yaichakaza Friends Rangers

Theresia Gasper -Dar es salaam

TIMU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-2, dhidi ya Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki uliochezwa  jana Uwanja wa Polisi, Kurasini, Dar es Salaam.

Yanga wanajipanga kucheza na timu ya Mbao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  utakaochezwa  Oktoba 22, mwaka huu, kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba, Mwanza.

Timu hiyo pia inakabiliwa na mchezo wa kuwania kufuzu makundi  ya Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya Pyramid ya Misri, unaopangwa  kuchezwa Oktoba 27, mwaka huu  katika dimba la CCM Kirumba.

Katika mchezo wa jana, mabao ya Yanga yalifungwa na Maybin Kalengo, David Molinga na Papy Tshishimbi.

Kalengo alifunga  dakika ya 23 kabla ya Molinga kufunga mawili dakika ya 24 na 27 huku Tshishimbi  akitupia  bao la nne dakika ya 32.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mratibu wa timu hiyo, Hafidh Salehe, alisema mchezo mwingine wanatarajia kuchezwa Jumatano  dhidi ya Pan African kwenye uwanja huo wa Polisi.

“Baada ya mchezo huu Jumatano tutacheza mwingine  ikiwa ni  moja ya kuwaweka wachezaji fiti fiti kabla ya kwenda Mwanza kuivaa Mbao,” alisema. Katika hatua nyingine, Hafidhi amesema beki wao Kelvin Yondan ambaye anasumbuliwa na jeraha  leo anatarajiwa kuanza mazoezi baada ya hali yake kuwa vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles