28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA YABANWA YATUA KILELENI

Sosthenes Nyoni

TIMU Yanga imelazimishwa suluhu na Gwambina,katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jana Uwanja wa Gwambina Complex, ulioko wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.

Hata hivyo, licha ya suluhu hiyo, Yanga ilichumpa hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kufikisha pointi 23, ilizozipata baada ya kushuka dimbani mara  tisa, ikishinda michezo saba na sare mbili.

Wakati huo huo Azam ambayo kabla ya suluhu ya Yanga ilikuwa ikishikilia uongozi wa ligi hiyo ikiwa na pointi 22, imeshuka hadi nafasi ya pili, baada ya kushuka dimbani mara tisa, ikishinda michezo saba, sare moja nakupoteza mchezo mmoja.

Kwa  upande mwingine, Gwambina baada ya  kuvuna pointi moja jana, inakamata nafasi ya 12, ikiwa na pointi 10, ikishuka dimbani mara 10, ikishinda michezo miwili, sare nne na kupoteza michezo minne.

Katika mchezo wa jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze aliwatumia baadhi ya wachezaji ambao hakuwa akiwapa nafasi katika michezo iliyopita, uamuzi uliotafsirika ni kuwaepusha na majeraha nyota wake wakati anasubiri kuikabili Simba Jumamosi hii Uwanja wa Mkapa.

Eneo la ulinzi la Yanga ndilo hasa lilikuwa na mabadiliko makubwa kwani badala ya kuwatumia Lamine Moro na Bakar Mwamnyeto, kucheza eneo la  ulinzi wa kati, jana aliwatumia Abdalah Shaibu na Said Juma Makapu, huku nafasi ya beki ya kulia akimtumia Paul Godfrey  badala ya Kibwana Shomary ambaye amekuwa akimtumia kwenye michezo iliyopita.

Katika eneo la kiungo, Feisal Salum amekuwa akitumika mara nyingi sambamba na Mukoko Tonombe, lakini Kaze aliwatumia Zawadi Mauya na Abdulaziz Makame.

Kwenye ushambuliaji alianza na Yacouba Sogne na Wazir Junior badala ya Michael Sarpong aliyeanzia benchi na kuingia kipindi cha pili.

Kwa ujumla, Yanga ilitawala sehemu kubwa ya mchezo wa jana na kufanya mashambulizi mengi, lakini kikwazo kilionekana kwa kipa wa Gwambina ambaye alionekana kuwa na siku nzuri kutokana na kuokoa michomo mingi.

Lakini Gwambina nayo haikuonyesha upweke kwani ilifanya mashambulizi kadhaa hasa kipindi cha kwanza, lakini iliporejea uwanjani baada ya mapumziko wachezaji wake walionekana kuchoka na kutumia mbinu ya kupoteza muda.

Mchezo mwingine uliopigwa jana, Biashara ikiwa nyumbani Uwanja wa Karume Musoma, ililazimishwa sare ya bao 1-1 na KMC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles