25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga ya Burundi yatwaa ubingwa

Na Winfrida Mtoi

Wakati Yanga ya Dar es Salaam ikishindwa kuchukua kombe mbele ya mtani wake Simba, timu ya mashabiki wa Wanajangwani hao ya nchini Burundi inayojulikana kama Yanga of Burundi, imefanikiwa kutwaa ubingwa katika fainali ya Mashindano ya Likizo ‘Tournoi Vacance 2021,’ zilizofanyika Jumapili Julai 25, mjini Bujumbura, nchini Burundi.

Katika mashindano hayo, Yanga ilifanikiwa kubeba kombe baada ya kuifunga New Bwiza kwa mikwaju 3-2 ya penalti baada ya kwenda sare ndani ya dakika 90.

Kikosi Yanga ya Burundi, kina baadhi  ya wachezaji wanaocheza na waliowahi kucheza timu za Tanzania kama vile Jonathan Nahimana(Namungo), Ally Niyonzima(Azam), Alex Kitenge(Stand United), Pierre Kwizera(aliwahi kucheza Simba) Emmanuel Mvuyekule(KMC)

Kiongozi wa timu hiyo, Mwami Ndjikile, amezungumza na Mtanzania Digital kutoka Burundi, amesema walicheza fainali siku ambayo Yanga ya Tanzania ilikuwa inacheza Kigoma na kufanikiwa kuchukua ubingwa huo.

“Jumapili sisi Yanga of Burundi, tumecheza fainali kama walivyocheza Yanga ya huko Tanzania, lakini bahati mbaya Yanga Tanzania imefungwa bao 1-0, ila sisi tumefanikiwa kubeba kombe la hapa Bujumbura mjini Kati,” amesema Njikile.

Ameeleza kuwa timu hiyo ilianzishwa muda mrefu tangu 2011 ndani ya tawi la mashabiki wa Yanga wa nchini humo na wamekuwa wakishirikiana na viongozi wa Klabu ya Yanga wa Tanzania.

“Tumetengeneza tawi la Yanga Burundi kwa sababu tunaipenda sana hii timu. Jina la Young maana yake vijana na sisi hapa tuna vijana wengi katika timu hii,” ameeleza Ndnjikile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles