31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA WATAMBA KUILIZA MBAO FC

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

YANGA leo wanatarajia kushuka dimbani kuumana vikali na Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Wanajangwani hao wanakutana na Mbao FC wakiwa na kumbukumbu na kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Yanga itashuka dimbani wakiwa wanahitaji ushindi kutokana na matokeo mabaya ya mechi mbili za kwanza.

Timu hizo zilipokutana msimu uliopita kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa, jijini hapa na waliporudiana CCM Kirumba, Wanajangwani hao walishinda mabao 2-1.

Mchezo huo wa leo utakuwa ni wa kisasi kwa upande wa Mbao FC, huku Yanga wakitaka kuendeleza rekodi nzuri katika dimba hilo la CCM Kirumba.

Yanga wataivaa Mbao wakiwakosa wachezaji wao, Mohammed Issa ‘Banka’ na Issa Bigirimana ambao ni majeruhi.

Upande wao Mbao FC, watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya bao 1-1 katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mwadui FC, uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, alisema wanakutana na Mbao timu ambayo huwa inawakamia sana lakini mipango yao ni kujituma zaidi na kupata pointi tatu muhimu.

“Tutakuwa makini zaidi kwenye mchezo huu kwani pia ni kama maandalizi kuelekea kwenye mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramid ili tuweze kupata ushindi,” alisema.

Upande wao Mbao FC, watakuwa wanahitaji ushindi baada ya kupata pointi moja kwenye mchezo wao wa mwisho walipokuwa ugenini.

Viingilio katika mchezo huo ni shilingi 5,000, sh 20,000 na sh 50,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles