26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga watamba kuigonga KMC

Mohamed Kassara – Dar es Salaam

BAADA ya kuzima tambo za watani wao wa jadi, uongozi wa Yanga umetamba kuwa shangwe za kuvuna pointi tatu zitaendelea kesho kwani lazima waichape KMC.

Pambano hilo linatarajia kupigwa  Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo timu hizo mbili zina maskani yao.

Yanga inaendelea kusherekea ushindi wa bao wa 1-0, ilioupata, katika mchezowa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja huo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga , Hassan Bumbuli, alisema ushindi huo umewapa morali mpya wachezaji wao na wameahidi kipigo kwa kila atakayepita mbele yao.

Alisema wamejipanga kushinda mchezo huo ili kuendelea kuwapa raha mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi na kuwapa hamasa ya kuichapa Simba.

 “Baada ya kuchukua pointi tatu zetu kwa Simba,sasa tunarudi kwa kasi kumalizia michezo yetu iliyobaki,ushindi wa derby umeamsha upya morali ya wachezaji, kila  mmoja wetu amefurahishwa na ushindi huo, hivyo tumekubaliana kuhakikisha tunashinda michezo yote iliyobaki.

 “Tunajua itakuwa mechi tofauti na iliyopita, KMC ni timu nzuri, hivyo tunaenda kwa tahadhari zote kuhakikisha pointi tatu zinakuwa upande wetu,”alisema Bumbuli.

Lakini Kocha Mkuu wa KMC, Haruna Harerimana, amempiga Bumbuli kwa kusema watahitimisha sherehe za Yanga kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Najua tuna mchezo mgumu mbele yetu dhidi ya Yanga, mechi hii ni muhimu sana kwetu kushinda ili kulinda morali ya wachezaji kujiamini kikosini, hivyo lazima tufanye kila tuwezalo kupata matokeo.

“Yanga imezidi kuimarika hasa baada ya kuifunga Simba, tunafahamu ubora wao na watakuja wakijiamini zaidi, tayari tumejipanga kuhakikisha tunakabiliana na presha yao, lakini la muhimu ni kupata pointi tatu na kujinusuru kutoka katika nafasi tuliopo kwa sasa kwenye msimamo wa ligi,

”alisema kocha huyo wa zamani wa Lipuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles