22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Yanga waishangaa Simba

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema hawajawekeza nguvu nyingi Kombe la Mapinduzi Zanzibar kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao, Simba, kwani akili zao zote zipo Ligi Kuu Tanzania Bara ili waweze kufanya vizuri na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Simba wameonyesha dhahiri kutaka kukutana na Yanga katika mchezo wa fainali au hata nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi ili waweze kupata ushindi baada ya kutoka nao sare ya mabao 2-2 mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumamosi iliyopita.

Katika mchezo huo, Simba ndio waliotangulia kwa kuwa mbele kwa mabao 2, lakini badaye Yanga walisawazisha yote ndani ya dakika tatu hali iliyowaumiza Wekundu wa Msimbazi na kujiona kama wamepoteza mechi hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema wana mechi nyingi za viporo ambazo wanahitaji kushinda zote hivyo hawawezi kuweka akili zao zote Mapinduzi Cup.

“Sisi hatuwezi kuweka nguvu nyingi sana huko japo tutapambana ili tupate ushindi katika mechi zetu, lakini nguvu na akili ni katika ligi, kama wapinzani wetu wametupania, basi tukutane kwenye ligi,” alisema.

Alisema wachezaji wao wamechoka wanahitaji kupata mapumziko hivyo watacheza mechi za Kombe la Mapinduzi, lakini si kwa nguvu kama wengine wanavyofikiria, hivyo kama Simba wanataka kuona muziki wao, wasubiri katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara.

Mwakalebela alisema mipango yao ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo watakuwa makini kuhakikisha wanashinda mechi zao zote.

Yanga jana usiku walitarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, huku Simba kesho wakiivaa Azam kwenye hatua hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles