26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga waanza kuwasoma Esperanca

playersNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga, leo wanatarajia kuanza kuwasoma wapinzani wao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Sagrada Esperanca ya Angola, kwa kuziangalia video za michezo iliyopita ili kusoma mbinu zao kabla ya  mchezo utakaochezwa Mei 7 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu hiyo kutolewa na Al Ahly katika  hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa jumla ya mabao 3-2 hali iliyopelekea kujumuishwa  na  timu nane zilizopoteza  michezo yao katika ligi hiyo ambazo zinatarajia kupambana na washindi  nane wa michezo ya Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na MTANZANIA jana Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jerry Muro,  alisema timu hiyo inatarajia kuweka kambi jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo huku benchi  la ufundi litakuwa makini kuzifuatilia kwa makini video za wapinzani wao.

“Hadi sasa wachezaji wote wapo salama na hakuna taarifa yoyote ya majeruhi, ingawa Simon Msuva alipata mchubuko kidogo katika mguu wake lakini haitazuia kutocheza kwenye mchezo huo.

“Wapinzani wetu tunawafahamu vizuri baada ya kuwafuatilia kupitia video zao za michezo iliyopita, hata hivyo safari hii benchi la ufundi litakaa chini ili kuziangalia kwa makini video hizo ili kusaidia kimbinu kabla ya kukutana nao,” alisema Muro.

Akizungumzia michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyobakia, Muro alisema wanatarajia kutangaza ubingwa kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumatano ijayo.

“Baada ya mchezo wa kimataifa Jumanne tutakuwa Mbeya kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya timu ya Mbeya City ambao pointi tatu tukizichukua zinaweza kutufanya kutangaza ubingwa kwenye mchezo huo.

“Kutokana na uimara wa kikosi chetu hakuna timu ya kutuzuia tusipate pointi tatu na kutufanya kutangaza ubingwa msimu huu,” alisema Muro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles