26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Yanga, Simba wapigana vijembe nje ya uwanja

simbayngNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba inatarajia kurejea Dar es Salaam leo wakitokea Zanzibar, huku watani zao Yanga wakitamba kufanya maaja bundani ya dakika 45 za mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho katika Uwanja waTaifa.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro, amesema kuwa kikosi chao kipo kamili kwa ajili ya mpambano huo na kudai kocha wao, Hans van Pluijm, amemaliza kazi ya kukiandaa kikosi hicho kumenyana na Simba.
“Kocha amemaliza kazi na kikubwa anataka mabao ya kutosha kipindi cha kwanza ili kuumaliza mchezo mapema.
“Wao wanajivunia historia ya kupata matokeo dhidi yetu, lakini wamesahau kuwa sekretarieti hii ni mpya, hivyo tutawaonyesha moto tuliokuja nao kwa kuwafunga siku hiyo,” alisema.
Alisema uwepo wa washambuliaji bora; Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngassa, Danny Mrwandana Simon Msuva kwenye kikosi chao, utaweza kuisambaratisha Simba.

Yanga ilianza mazoezi ya kuivaa Simba Jumatatu iliyopita kwenye kambi yao waliyoweka Bagamoyo, mkoani Pwani.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba, IddKajuna, alisema kikosi chao kitarejea Dar es Salaam leo kikiwa kamili tayari kwa kuivaa Yanga.
“Tumemaliza kazi ya kuifunga Yanga, maandalizi yote yamekamilika, Mungu akipenda kesho (leo) tutaanza safari ya kurejea Dar es Salaam, kocha amewanoa vema vijana na wako tayari kuilaza Yanga Jumapili,” alisema.

Simba nayo ilianza kuiwinda Yanga, Jumatatu iliyopita mjini Unguja, walipoweka kambi katika nyumba kubwa ya mwanachama mmoja wa timu hiyo iliyopo Chukwani.
Mchezo wa kwanza wa ligi uliofanyika Oktoba 18, mwaka jana timu hizo zilitoka suluhu, lakini Simba ilimfungaYanga mabao 2-0 kwenye mechi maalumu ya Nani Mtani Jembe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles