27.1 C
Dar es Salaam
Sunday, December 15, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga salama salmini

Na WINFRIDA MTOI – DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umewataka wanachama na wadau wake, kupuuza taarifa zinazosambazwa na mmoja wa wanachama  wao, kuwa mdhamini  wa timu hiyo, Kampuni ya GSM ina mpango ya kuikacha.

Taarifa ya GSM kujitoa kuidhamini Yanga, ilisambaa juzi, ikidaiwa hatua hiyo inatokana yaliyojiri katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na wadhamini hao.

Baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, uongozi wa Yanga kupitia  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli, jana ulijitokeza na kukanusha kuwapo kwa mpango wa GSM kujiondoa kuwadhamini.

Bumbuli alisema hakuna mgogoro wowote  kati ya klabu yao na GSM, hivyo taarifa zinazoenezwa ni uzushi wenye lengo baya na maendeleo yao.

Alisema wanasikitishwa na taarifa iliyotolewa na mwanachama huyo, ikionekana ina lengo la kuwagawa Wanayanga, hasa baada ya timu yao kuwa na mwenendo mzuri.

 Alieleza kikao chao kilikuwa na ajenda nyingi, lakini kubwa ilikuwa kuangalia maendeleo ya klabu yao.

“ Kwa kawaida kikao cha Kamati ya Utendaji  kinatakiwa kufanyika mara nne kwa mwaka na juzi kilikuwa cha kwanza kwa mwaka huu wa 2020, kikiwa na lengo la kujadili maendeleo.

“Kulikuwa na ajenda nyingi na hakijamjadili mdhamini yoyote, taarifa iliyotolewa na mwanachama wetu ni kutaka kutugawa Wanayanga zipuuzwe, Yanga iko vizuri, hakuna mgogoro,”alisema Bumbuli.

Alisema katika kikao hicho, pia  walijadili  uanzishwaji wa jarida la Yanga,  ili kuwapa fursa ya kupata habari za klabu yao wapenzi , Wanayanga na mashabiki wa timu hiyo na kuweka mikakati ya miaka mitatu ijayo.

“Pia kikao kilikuwa na lengo la kuwasilisha taarifa za sekretarieti, yaani sisi tangu tumeingia Yanga tumefanya nini, hivyo wanachama wetu wazipuuze na kuendelea kushikamana,” alisema Bumbuli.

Alisema kitu kingine kikubwa walichojadili ni kujipanga kurejea kwa kishindo katika Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), pale Serikali itakaporuhusu shughuli za michezo kuendelea baada ya zuio la siku 30, ikiwwa ni tahadhari ya kuenea kwa virusi vya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles