27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Yanga Princess yazitaka pointi sita Kanda ya Ziwa

Glory Mlay -Dar es Salaam

KOCHA Msaidizi wa Yanga Princess, Nasoro Mukhsin, amesema wamepanga kuondoka na pointi zote sita Kanda ya Ziwa.

Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Februali 4 kuumana na TSC Uwanja wa Gwambina  kabla ya kuikabili Alliance Februari 7, Uwanja wa Nyamagana, ikiwa ni michezo ya Ligi Kuu ya soka ya Wanawake Tanzania Bara.

Timu hizo mbili zote zina maskani mkoani Mwanza.

 4 katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Gwambina kabla ya kukutana na Alliance Girls kwenye mchezo utakaochezwa Februari 7 , Nyamagana.

Akizungumzia mchezo wao na TSC, Mukhsin alisema, wanatambua  TSC ni timu imara, lakini watapambana ili kupata matokeo chanya.

“Hatukupata matokeo ya ushindi kwenye mechi yetu na JKT Queens  hivyo lazima tupambane kusaka pointi tatu.
 “Kwa sasa tunaendelea na mazoezi Uwanja wa JMK Park , kikubwa ni kuona namna gani tunaweza kupata pointi tatu, mashabiki watupe sapoti kwa kujitokeze kwa wingi, tupo karibu kunusa tatu bora kwenye msimamo, ” alisema.

Mukhisn alisema wanatambua ugumu wa ligi hiyo kwani kila timu inapambana kufanya vizuri hivyo hawatamdharau mpinzani wao yeyote.

Yanga ipo nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 12, baada ya kucheza michezo saba, ikishinda minne na kupoteza mitatu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles