27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga ndi ndi ndi

Juma Abdul

Na Seleman Shineni-Ghana

MATUMAINI ya Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika yamepotea, baada ya jana kufungwa mabao 3-1 na timu ya Medeama ya Ghana, katika mchezo wao wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Ghana Essipong Sport uliopo katika mji wa Takoradi.

Yanga ambayo inaendelea kushika mkia katika Kundi A kwa kuwa na pointi moja, ilikuwa ikicheza mchezo wake wa nne wa kundi hilo linaloongozwa na TP Mazembe yenye pointi saba, ikifuatiwa na Mo Bejaia yenye pointi tano na Medeama ambayo baada ya mchezo huo ilifikisha pointi tano.

Wenyeji Medeama ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao dakika ya 7 kupitia kwa beki, Daniel Amoah, aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Eric Kwakwa.

Beki huyo, mshambuliaji Enock Atta na kiungo, Kwesu Donsi, wanawaniwa na Azam, kwa ajili ya kuwatumia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na huenda wakatua nchini mara moja kumalizana na Azam.

Amoah dakika ya tisa nusura aiandikie Medeama bao la pili kwa njia ya penalti, lakini Kipa Deogratius Munishi alipangua penalti hiyo. Medeama ilipata penalti hiyo baada ya beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumwangusha mchezaji wa timu hiyo.

Hata hivyo, Medeama iliendelea na kasi yake ile ile na kufanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 22, kupitia kwa mchezaji wao, Abass Mohamed na kuiacha Yanga iliyoamini Medeama timu rahisi ikishangaa.

Bao hilo liliizindua safu ya ushambuliaji ya Yanga, iliyofanya mashambulizi makali yaliyosababisha mshambuliaji wake, Obrey Chirwa, kuchezewa rafu, hivyo kupata penalti iliyofungwa na Simon Msuva katika dakika ya 24 na kuzaa bao la kwanza.

Bao hilo ni kama liliichongea Yanga, kwani Medeama ilizidisha kasi ya kushambulia lango lake na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 37 kupitia kwa Abass.

Hadi mwamuzi Redouane Jiyed kutoka Morocco anapuliza filimbi kuashiria mapumziko, Yanga tayari ilikua imechapwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambualiana kwa zamu huku zikiimarisha ulinzi, Kocha Pluijm alifanya mabadiliko kwa kumtoa Yondani na kumwingiza Vicent Andrew, pia alimtoa Haruna Niyonzima na kuingia Juma Mahadhi.

Dakika ya 90, Simon Msuva alishindwa kufunga bao akipiga shuti kali ambalo liligonga mwamba.

Medeama: Daniel Agyei, Daniel Amoah, Malik Akowuah, Eric Kwakwa, Enock Agyei, Amoses Sarpong, Samuel Adade, Abass Mohamed, Paul Aidoo, Benard Danso na Kwesi Donso.

Yanga: Deogratius Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Nadir Haroub  ‘Canavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa na Harouna Niyonzima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles