24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga kupanga mauaji ya Zesco Mwanza

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga, kinatarajia kwenda Mwanza, Septemba 4 mwaka huu, kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wao wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco.

Mchezo kati ya timu hizo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga ilitinga hatua hiyo, baada ya kuiondosha mashindanoni timu ya Township Rollers ya Botswana, kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1.

Timu hizo zilipokutana Agosti 10,  Uwanja wa Taifa,  Yanga ililazimisha sare ya bao 1-1, lakini  zilipokutana katika mchezo wa marudiano uliochezwa Agosti 24 jijini Gaborone vijana hao wa  Jangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Salahe, alisema kwa sasa wanaendelea na programu ya mazoezi, huku wakipanga kwenda Mwanza kuweka kambi ya kuiwinda Zesco.

“Timu inatarajia kwenda Mwanza, Septemba 4, kuweka kambi, lakini vile vile tutacheza kama mechi mbili za kirafiki ikiwemo pia dhidi ya Pamba  ili kujiweka fiti kabla ya kuvaana na Zesco,” alisema.

Alisema wachezaji wao wanaoendelea na mazoezi ni wale ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu za taifa zinazojiandaa na michezo ya kusaka nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Hafidhi alisema mikakati wanayoipanga wanaamini itawasaidia kuendelea kupata matokeo mazuri na kusonga mbele.

Tanzania  imesaliwa na timu mbili katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika(Caf), ambazo ni  Yanga inayoshiriki Ligi ya Mabingwa na Azam FC,  Kombe la Shirikisho.

Awali ilikuwa na timu nne, nyingine ni Simba iliyokuwa inashiriki Ligi ya Mabingwa kabla ya kutupwa nje na UD Songo ya Msumbiji na KMC iliyoondolewa Kombe la Shirikisho na AS Kigali ya Rwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles