26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Yanga kumwaga mil. 200/-

Zainab Iddy na Mohamed Kassara

KATIKA kuonyesha Yanga imedhamiria kupata ushindi mbele ya Simba, mdhamini wa klabu hiyo, kampuni ya GSM, wametenga kitita cha sh milioni 200 kwa wachezaji iwapo wataondoka na alama tatu.

Yanga inataraji kuwakaribisha Simba kesho kutwa (Jumapili) katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara utajkaopigwa ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hizo zitaingia Uwanjani zikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mechi ya mzunguko wa kwanza ambako Simab ndio waliokuwa wa kwanza kuziona nyavu za Yanga kabla ya Wanajangwani kuja kuyarejesha.

Akizungumza katika Makao makuu ya klabu hiyo yaliopo Jangwani, Dar es Salaam, Ofisa Muhamasishaji wa Yanga, Antony Nugaz, alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetolewa na GSM ikiwa ni sehemu ya pongezi kama timu yao itashinda.

“Hii mechi ni muhimu sana kwa wachezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla kwani zimewekwa milioni 200 zitakazogawanywa kwa wote, lakini bado kuna mchezaji wa Yanga atakayetoa mchango mkubwa siku hiyo ana fungu lake.

“Tunahitaji ushindi kwa hali na mali kwa sababu tunahitaji heshima mbele ya Simba, hata kama ikitokea tukashindwa kuchukua ubingwa msimu huu, kuwafunga Simba itakuwa ni faraja kwetu,” alisema.

Wakati huo huo, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, imesema imejipanga kuwahakikishia usalama mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mpambano huo keshokutwa.

Tamko hilo limetolewa na baada ya kikao cha pamoja kati ya Mkurugenzi wa Michezo, Omari Singo, Jeshi la Polisi, Bodi ya Ligi na wawakilishi wa klabu hizo ili kuweka sawa mikakati ya ulinzi wakati wa mchezo huo.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Singo alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wote wanaohusika na maandalizi ya mchezo huo, wamekubaliana kuhakikisha mashabiki watakaojitokeza uwanjani hapo wanaingia na kutoka salama.

“Serikali, Bodi ya Ligi, jeshi la Polisi, kwa pamoja tumefanya kikao kilichojadili mbinu mbalimbali za kurahisisha usalama mashabiki watakaojitokeza, tunajua mchezo huo ni mkubwa na umekuwa na matukio ya hapa na pale, lakini safari hii tumejidhatiti kudhibiti fujo ili watu wafurahie mchezo.

“Tumeandaa utaratibu rahisi utakaowafanya mashabiki kuingia uwanjani bila bughudha, tunaomba mashabiki waache mazoea ya kuingia uwanjani muda mfupi kabla ya mechi kuanza, waingie mapema ili kuepusha fujo zisizo za lazima ambazo hutokea kutokana na watu kuchelewa kuingia uwanjani.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kisongo aliwataka Watanzania kujitokea kwa wingi uwanjani ili kumfanya mgeni rasmi wa mchezo huo, Raisi wa Shirikisho la Soka Afrika, Ahmad Ahmad ukubwa wa mchezo huo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,509FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles