27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuandika historia leo

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga inatarajia kuandika hitoria mpya leo ya kusaini mkataba na Kampuni ya La Liga ya nchini Hispania, itakayosaidia katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Hafla ya utiaji saini mkataba huo itafanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni na kushuhudiwa na watu mbalimbali.

Mkataba huo ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na wadau wa klabu hiyo baada ya kushindwa kusainiwa mapema kutokana na janga la Corona lililozuia shughuli zote za michezo.

Akizungumzia mkataba huo kupitia tovuti ya Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, David Luhango, alisema wataalamu wa La Liga watashirikiana na Kamati ya Mabadiliko ili kupata mfumo sahihi.

Alisema wataalam hao wataweka kambi nchini, wakiwezeshwa na GSM kutekeleza majukumu yao hadi mchakato utakapokamilika.

“Tunaamini ushirikiano huu na La Liga utaleta tija kubwa, watatuongoza katika njia iliyobora zaidi kuelekea katika mafanikio kutokana na uzoefu wa uendeshaji wa timu na soka la kisasa,” alisema Ruhago.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Hassan Bumbuli, amethibitisha kurejea kwa kipa wao Farouk Shikalo na kuungana na kikosi mazoezini jana.

Tangu Ligi Kuu Tanzania Bara ilivyosimama kutokana na janga Corona, Shikalo alikuwa kwao nchini Kenya ambako mipaka ilifungwa lakini jana alifanikiwa kuwasili nchini.

Bumbuli alisema Shikalo ameungana na wenzake walioanza mazoezi tangu Jumatano wiki hii kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam.

“Yanga hatuna mchezaji mwingine aliopo nje, kikosi kimekamilika baada ya Shikalo kuwasili leo (jana), tunaendelea na maandalizi ya mechi zetu ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘Azam Federation Cup,” alisema Bumbuli.

Alisema malengo ya Yanga ni kuhakikisha inashinda mechi zote zilizobaki ili kujiweka katika njia sahihi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

“Kikosi kipo chini ya Kocha Msaidizi, Charles Mkwasa, wachezaji wapo fiti hakuna majeruhi, tunachotaka ni kushinda mechi zote za ligi na kombe la shirikisho.

“Hata kama hatutachukua ubingwa wa Ligi Kuu, lazima tushinde mechi zetu, haiwezekani uchukue ubingwa wa Kombe la Shirikisho halafu katika Ligi umalize nafasi za chini, kote tunataka kuwa juu,” alisema Bumbuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles