24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kamili Algeria

Yanga-lineNA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, timu ya Yanga kesho itaivaa timu ya Mouloudia Olympique Bejaia, katika Uwanja wa Unite Maghrebine, nchini Algeria.

Yanga itakuwa ikicheza mechi hiyo huku Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), likiwaongezea nguvu kwenye kikosi chao baada ya kuruhusiwa kuwatumia wachezaji wake wapya wanne, kipa Benno Kakolanya, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, Vincent Andrew na Juma Mahadh.

Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco, Bouchaib El Ahrach, akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabrouk.

Yanga wamewasili nchini Algeria jana wakitokea Uturuki ambapo waliweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, ameliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa wanashukuru wamewasili salama nchini Algeria huku wachezaji wao wakiwa katika ari ya ushindi na pia kuruhusiwa kwa wachezaji wao wapya kucheza mechi hiyo.

“Tunashukuru tumewasili salama, lakini pia kitendo cha kuruhusiwa kwa wachezaji wetu wanne  na  kuwajumuisha katika mechi yetu na Mo Bejaia ni faraja kubwa na imeongeza chachu kwa kikosi kizima,” alisema.

Juzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lilipokea barua kutoka Shirikisho la  Soka Afrika (CAF) likitoa ruhusa kwa Yanga kuwatumia wachezaji hao.

Huenda kuruhusiwa kwa wachezaji hao kukaleta matumaini kwa Yanga kutokana na kuwepo pengo kwa baadhi ya nafasi kufuatia Juma Abdul kuwa majeruhi na Nadir Haraub ‘Cannavaro’ kutumikia adhabu ya kadi nyekundu na hivyo kulazimika kuukosa mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa Yanga imetinga hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya pili tangu walipofanikiwa kufanya hivyo mwaka 1998.

Mara baada ya mchezo huo, Yanga iliyo Kundi A itarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi yake dhidi ya TP Mazembe Juni 28 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi kilichowasili Algeria kinajumuisha makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Benno Kakolanya na Deogratius Munishi ‘Dida’.

Mabeki; Hassan Kessy, Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan,  Pato Ngonyani, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Vicent Bossou.
Viungo; Juma Mahadhi, Thabani Kamusoko, Said Juma ‘Makapu’, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.Washambuliaji; Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Matheo Anthony.

Kocha mkuu, Hans van der Pluijm, Kocha msaidizi, Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, mchua misuli, Jacob Onyango, mtunza vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles