Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
YANGA ni kati ya timu zilizofanya usajili wa wachezaji wengi katika kipindi hiki kuboresha kikosi chake kuelekea msimu wa 2021\2022.
Usajili huo umezingatia upungufu ulioonekana msimu uliopita ambapo imeshindwa kuchukua ubingwa wamashindano yote, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.
Hali hiyo iliwanyong’onyesha mashabiki wake ambao waliaminishwa kuwa watachukua ubingwakatika msimu huo kutokana na usajili waliofanya lakini matokeo yake mambo yakaenda tofauti.
Ukiangalia katika msimu uliopita Yanga ilifanya usajili wa wachezaji wengi tena waliotua kwa mbwembwe zote na kufanyiwa mapokezi makubwa na mshabiki.
Kuelekea msimu mpya Wananchi hao wamefanya tena kufuru ya usajili na kuachana na baadhi ya nyota wake ikiwamo makipa wawili waliokuwa waliokuwa tegemeo kikosini, Metacha Mnata na Farouk Shikalo.
Katika maboresho ya msimu mpya mbao wanajangwani hao watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kuna maingizo mapya zaidi ya 10.
Wachezaji hao ni Yusuph Athuman,Fiston Mayele,Heritier Makambo, Shaban Djuma Djigui Diarra,Khaleed Aucho,Eric Johora, Dickson Ambundo,David Bryson,Jesus Moloko na Yannick Bangala.
Usajili huo ni mzuri kulingana na historia ya wachezaji hao kwa kilewalichokifanya katika timu wanazotoka, huku Makambo akiaminiwa zaidi kufanya vizuri kutokana na rekodi yake Jangwani.
Pamoja na yote hayo, uongozi wa Yanga unatakakiwa kutambua kuwa bado haujamaliza kazi, hasa ukizingatia inakabiliwa na michuano ya kimataifa.
Ni vizuri Wanangwani hao wakatazama nyuma na kuweka mikakati mipya ya kuingia katika msimu mpya kwa sababu kusajili pekee hakuwezi kuifanya timu bora.
Yapo mambo mengi yanahitajika ili kukifanya kikosi kiwe bora na ushindani ikiwamo kuweka msingi na malengo kwa kufanya vitendo na si maneno.
Ikumbukwe msimu uliopita kulikuwana mamneno mengi ya kuwaamninisha wadau kuwa Yanga ni bora, imefanya usajili hivyo ubingwa ni lazima.
Kama Yanga inataka kufanya vizuri Kimataifa na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, basi uongozi ujipange zaidi, hata kwa kuangalia watani zao walifanya nini hadi kufanikiwa kufika robo fainali mara mbili katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Uongozi utambue kuwakwa sasa mashabiki wao wanahitaji makombe na kufanya vizuri Kimatiafa na si maneno bali vitendo.
Katika kutambua kuwa Wanajangwani hao wana deni na kiu ya wadau wao kuona kikosi bora, ni umati uliojitokeza jana katika kilele cha Wiki ya Wananchi na maoni mbalimbali waliyotoa.
Ili kulinda rasilimali hiyo ya watu kama kauli mbiu inavyosema kuwa ‘Sisi tuna Watu’, lazima iambatane na matokeo mazuri uwanjani.