25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga hiyoo Misri, matumaini kibao

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga kinarajia kuondoka leo kwenda Misri, huku wachezaji wakitamba kupambana mwanzo mwisho kuhakikisha wanashinda mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya huko, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili.

Yanga wanakwenda Misri wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ya mtoano uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kikosi hicho kinaondoka kikiwa na jeshi la wachezaji 20, ambao ni makipa Farouk Shikalo, Metacha Mnata na Ramadhan Kabwili, huku mabeki wakiwa ni Juma Abdul, Ally Ally, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro na Mharami Issa ‘Marcelo’.

Viungo ni Papy Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mapinduzi Balama, Abdulaziz Makame, Deus Kaseke, Jaffar Mohammed, huku mawinga wakiwa ni Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, wakati washambuliaji ni Sadney Urikhob na Juma Balinya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Balinya alisema anaamini timu yake itafanya vizuri japo mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tulifanya makosa mchezo wa awali, lakini naamini tutaweza kupambana katika mechi ya marudiano na kupata matokeo kama wao walivyopata ugenini,” alisema.

Kwa upande wake, Sonso alisema wanakwenda Misri wakiwa na matumaini ya kushinda na kusonga mbele kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha, hivyo tunakwenda tukiwa na mbinu mpya ya kupata matokeo mazuri,” alisema.

Yanga inatakiwa ikapate ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili waweze kusonga mbele katika michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles