Yanga: Hatushindwi

0
1697
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Simai Mohammed Said salimiana na wachezaji wa Yanga wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao kuangalia mazoezi kwenye Uwanja wa Likidi nchini Botswana jana.

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

WACHEZAJI wa Yanga wakiwa kambini nchini Afrika Kusini, wameahidi kupambana kwa kila namna kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele, katika mchezo wao wa marudiano wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Mchezo wa marudiano kati ya Yanga na Township utapigwa kesho kutwa jijini Gaborone.

Timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Agosti 10, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ililazimishwa sare ya bao 1-1.

Hii ina maana kwamba mchezo wa marudiano utakuwa mgumu zaidi hasa kwa Yanga kutokana na kuruhusu bao la ugenini, kwani itakazimika kusaka ushindi au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kutinga raundi ya kwanza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MTANZANIA jana kwa simu kutoka Afrika Kusini, walisema bado wana matumaini ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo na kusonda mbele.

“Haina jinsi itatubidi tupambane ili tushinde,  kama wao waliweza kupata bao kwetu vile vile na sisi tunaweza kupata ushindi kwao, kocha amekaa na sisi na kutuelekeza kile tunachotakiwa kufanya ugenini,” alisema.

Kwa upande wake, mshambuliaji wa timu hiyo, Juma Balinya alisema wanafahamu hitaji la mashabiki wa Yanga ni kuona kikosi chao kilipata ushindi na kusonga mbele, hivyo wamejiandaa kwa mapambano ili kuwatimizia aja yao.

“Tumejiandaa kwa ajili ya kupambana na kushinda, tutahakikisha hatufanyi makosa kwa mara nyingine, nawaomba mashabiki wa  Yanga watuamini,” alisema mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu ya Uganda msimu uliopita akiwa na timu ya Polisi ya nchi hiyo.

Naye beki, Ally Sonso alisema kutokana na maandalizi ya uhakika ambayo wamekuwa wakifanya kwa ajili ya mchezo huo, wana kila sababu ya kuibuka na ushindi dhidi ya wenyeji wao.

“Tunafanya maandalizi ya uhakika lengo likiwa kupata matokeo mazuri na kusonga mbele, kila mmoja anafahamu kwamba hii ni vita na ili kushinda lazima kila mmoja atomize wajibu wake.

“Kwa upande wetu wachezaji tumejiandaa kwa hili, tunafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini nathubutu kusema tuko vizuri,”alisema beki huyo wa zamani wa Lipuli ya Iringa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here