33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA, AZAM DIMBANI ZANZIBAR LEO

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


azamTIMU ya soka ya Yanga, leo itatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi itakaposhuka dimbani kumenyana na Jamhuri ya Pemba katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar huku Azam ikivaana na Zimamoto.

Mchezo wa Wanajangwani hao ambao wamepangwa Kundi B, unatarajiwa kuchezwa saa 2:30 usiku baada ya kuanza pambano la Azam na Zimamoto saa 10:00 jioni.

Yanga wanashiriki mashindano hayo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kuondoshwa katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita na mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya URA ya Uganda kwa mikwaju ya penalti 4-3.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mzambia, George Lwandamina, kitaingia uwanjani bila beki wake mahiri, Vicent Bossou, aliyekwenda kuiwakilisha timu yake ya Taifa ya Togo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika nchini Gabon Januari mwaka huu.

Akizungumzia mashindano hayo, Katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Baraka Deusdedit, alisema watatumia michuano hiyo kujiimarisha zaidi kwa michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ina ushindani mkubwa msimu huu.

Kwa upande wa Azam kikosi chao kitaongozwa na makocha wazawa waliopandishwa kutoka timu ya vijana, Idd Cheche, akisaidiwa na Idd Abubakar anayewanoa makipa.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Azam, Saad Kawemba, alisema watashiriki kwenye mashindano hayo kikamilifu licha ya kuwa katika kipindi kigumu tangu walipolivunja rasmi benchi la ufundi la timu hiyo.

Wiki iliyopita uongozi wa Azam ulitangaza kuwatimua makocha wake wote kutoka nchini Hispania waliokuwa katika benchi la ufundi kutokana na timu hiyo kufanya vibaya tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.

Alisema pamoja na kuwa katika kipindi cha mpito wanatarajia kufanya vizuri kwenye Kombe la Mapinduzi kwa sababu timu ipo salama na wachezaji wana ari kubwa ya kupata ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles