30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

YAJUE MATAIFA 10 GHALI YATAKAYO ONYESHANA KAZI URUSI

MOSCOW, Urusi


MAMBO yanazidi kupamba moto kuelekea fainali za kombe la dunia zinazotarajiwa kupigwa Urusi kwa mara ya kwanza nchini humo kuanzia Juni 14 mwaka huu  .

Tayari mataifa yaliyopata nafasi ya kushiriki fainali hizo yameweka wazi majina ya wachezaji wao ambao wataipeperusha bendera ya taifa hilo.

Achana na timu zinazopewa nafasi  ya kutwaa taji hilo linaloshikiriwa na timu ya Taifa ya Ujerumani, ambao wamekuwa wakipewa nafasi ya kutwaa tena kombe hilo.

Mjadala uliopo hivi sasa kwa wadau wa soka ni mataifa 10, ghali ambayo yataonyeshana umwamba katika mashindano hayo ambayo yanachukua mwezi mmoja .

1.Brazil  Euro milioni 673.50

Wakali hao wa Samba ndio vinara katika orodha hiyo  wanakadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni 673.50 ambazo ni sawa na Trilioni 1,803,220,000,000 za Kitanzania.

Hii  inachangiwa  asilimia 88 ya wachezaji wa timu hiyo kucheza soka nje ya taifa lao.

Mchezaji  ghali katika kikosi hicho ni Neymar dos Santos, ambaye anakipiga katika klabu ya PSG akiwa na thamani ya Euro milioni 150.

  1. Ujerumani Euro milioni 636.50

Mabingwa watetezi wa taji la kombe la dunia wanashika nafasi ya pili katika orodha ya mataifa ghali wakiwa na thamani ya Euro milioni 636.50 ambazo ni sawa na Trilioni 1,704,080,000,000.

Hii  inachangiwa na asilimia 41.7 ya wachezaji wake kucheza nje ya nchi hiyo.

Mchezaji ghali katika kikosi hicho ni winga wa Manchester City, Leroy Sane ambaye ana thamani ya Euro milioni 50.

  1. Ufaransa Euro milioni 636.50

Wakali hao ambao miaka ya karibuni wamekuwa wasindikizaji katika fainali za kombe la dunia wanashika nafasi ya tatu  wakiwa na thamani ya Euro milioni 636.50 ambazo ni sawa Trilioni 1,704,080,000,000 za Kitanzania.

Hii  inachangiwa na asilimia 58.3 ya kikosi hicho kukipiga nje ya Ufaransa.

Mchezaji ghali katika kikosi hicho ni Ousmane Dembele ambaye amejiunga na FC Barcelona kwa dau la Euro milioni 110.

  1. Hispania Euro milioni 603.50

Mabingwa hao wa kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini,  wanashika nafasi ya nne katika orodha ya timu zenye fedha nyingi wakiwa na  thamani ya Euro milioni 603.50 ambazo ni sawa na Trilioni 1,615,660,000,000 za Kitanzania.

Hii  inachangiwa na asilimia 41.7 ya kikosi chao kucheza nje ya Laliga.

Mchezaji ghali katika kikosi hicho ni mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata, ambaye ana thamani ya Euro milioni 30.

  1. Argentina Euro milioni 528.50

Vijana wa Jorge Sampaoli ambao walipoteza fainali za kombe la dunia nchini Brazili, mbele ya Ujerumani, wana thamani ya Euro milioni 528.50 ambazo ni sawa na Trilioni 1,414,710,000,000 za Kitanzania.

Hii  inatokana na asilimia 84.6 ya wachezaji kucheza soka nje ya taifa hilo.

Mchezaji ghali katika kikosi hicho ni mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, ambaye ana thamani ya Euro milioni 130.5.

6.Ubelgiji Euro milioni 503.75

Wakali hao ambao wamekuwa wakipewa nafasi ya kufanya vizuri nchini Urusi, wana thamani ya Euro milioni 503.75 ambazo ni sawa na Trilioni  1,347,720,000,000  za Kitanzania.

Hii  inachangiwa na asilimia 92.3 ya wachezaji kucheza soka nje ya Ubelgiji.

Mchezaji mwenye thamani zaidi katika kikosi hicho ni mshambuliaji wa Chelsea , Eden Hazard, ambaye ana thamani ya Euro milioni 75.

  1. England Euro milioni 339.00

Mabingwa wa mwaka 1956 wamekuwa wasindikizaji kwa muda mrefu wanashika nafasi ya saba katika orodha wakiwa na thamani ya Euro milioni 339.00 ambazo ni sawa na bilioni  908,307,000,000 za Kitanzania.

Hii  inachangiwa na asilimia 4.3 kucheza nje ya England.

8.Croatia Euro milioni 294.75

Wababe wengine kutoka kundi D ambao licha ya kutotajwa tajwa ni miongoni mwa mataifa ya kuchungwa zaidi msimu huu wanashika nafasi ya nane wakiwa na thamani ya Euro milioni 294.75 ambazo ni sawa na bilioni 787,735,000,000 za Kitanzania.

Hii  inachangiwa na asilimia 87.0 ya kikosi chao kucheza soka nje ya nchi yao.

9.Ureno Euro milioni 279.05

Mabingwa hao wa michuano ya ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa ni miongoni mwa mataifa ya kuchungwa, wakali hao wanashika nafasi ya tisa wakiwa na thamani ya Euro milioni 279.05 ambazo ni sawa na bilioni 747,545,000,000 za Kitanzania.

Hii  inachangiwa na asilimia 70.8 kucheza soka nje ya Ureno.

Mchezaji ghali katika kikosi hicho ni bingwa mara tano wa tuzo za Ballon d’or, Cristiano Ronaldo ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni 130.5.

10.Poland Euro milioni 220.33                                                     

Funga dimba ni timu ya taifa ya Poland ambayo ina thamani ya Euro milioni 220.33  ambayo ni sawa na bilioni 589,462,000,000 za Kitanzania,  hii inatokana na asilimia 64.3 ya wachezaji wake kucheza soka barani Ulaya.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles