24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Xavi ampeleka Mahrez Barca

riyad-mahrez-570882-600x338BARCELONA, Hispania

MCHEZAJI wa zamani wa Barcelona, Xavier “Xavi” Hernández, amesema kuwa anaamini mchezaji wa timu ya Leicester City ya Ligi Kuu England, Mahrez, atakuwa na mafanikio zaidi endapo atajiunga na  miamba ya Hispania, Barcelona.

Xavi alitoa kauli hiyo alipokuwa  akizungumza na televisheni ya Arby Al Jadeed ya Dubai, kwamba mchezaji huyo amefanikiwa kuwa bora  na kuwavutia wakongwe mbalimbali, akiwamo Xavi, ingawa  alikiri hakuwahi kumfuatilia kabla.

Kauli hiyo inakuja huku mashabiki wa klabu hiyo wakitaka wachezaji mahiri kwenye klabu hiyo, Leicester msimu huu.

Mchezaji huyo alijiunga na klabu hiyo Januari mwaka juzi, akitokea klabu ya Le Havre kwa mshahara wa pauni 400,000.

Mafanikio yake yaliongezeka zaidi akiwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Jamie Vardy (25) na kujikuta akifunga mabao 18 katika msimamo huu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles