25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

World Vision yazindua mradi wa kupambana na minyoo, kichocho Itilima

Derick Milton, Simiyu

Shirika la World Vision Tanzania limezindua mradi wa kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwemo Minyoo na Kichocho katika Wilayani Itilima.

Kwa mujibu wa Shirika hilo kupitia utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya nchini, Wilaya hiyo imekuwa na kiwango cha juu ya asilimia 30 cha maambukizi ya minyoo na kichocho, hali inayosababishwa na uhaba wa upatikanaji wa maji safi na mazingira salama Wilayani humo.

Mbali na hilo Idara ya Afya katika Wilaya hiyo inasema kuwa wananchi wengi wamekuwa na imani potofu juu ya dawa za Minyoo na kichcho wanazopewa pindi wanapopimwa na kukutwa na magonjwa hayo hali ambayo imesababisha pia kiwango cha maambukizi kuwa juu.

Mwakilishi wa Shirika hilo Rise Liwa akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huo amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu na utagharimu kiasi cha Dola za Marekani 864,993.00 sawa na Sh. Bil 1.9 za kitanzania chini ya ufadhili wa Serikali ya Korea(KOICA).

Liwa amesema kuwa shirika hilo linatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia ,Wazee na watoto pamoja na ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Arnold Musiba amesema hali ya magonjwa hayo si nzuri kutokana na jamii kubwa ya wakazi wa Wilaya hiyo kuwa na imani potofu juu ya dawa zitolewazo za minyoo na kichocho.

Kupitia mradi huo Wordvison itawafikia wananchi 283,972, kata 22, vijiji 102, vitongoji 587 na Kaya 44,171 ambapo shughuli mbalimbali za utoaji dawa za minyoo na kichocho zitafanyika, uchimbaji na usambazaji maji kwa vijiji 10 na uhamasishaji wa usafi wa mazingira kupitia viongozi wa maeneo husika na matumizi ya vikundi vya sanaa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,207FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles