24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

World Vision yatoa msaada vifaa vya kujikinga na corona mkoani Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Shirika la World Vision Tanzania limetoa msaada wa kujikinga na virusi vya corona likiwemo jengo la zahanati kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu, vyenye thamani ya Sh milioni 95.7 lengo likiwa kuboresha huduma za afya mkoani humo.

Msaada huo umekabidhiwa na Meneja wa shirika hilo Kanda ya Nzenga yenye mikoa ya Tabora, Shinyanga na Simiyu, John Massenza na kupokelewa na Katibu tawala wa Mkoa huo, Jumanne Sagini.

Massenza amesema katika msaada huo World Vision imetoa vifaa mbalimbali katika mkoa huo kwa ajili ya kupambana na virusi hivyo ambavyo ni glovu boksi 500, vitakasa mikono lita 200, barakoa na mavazi maalumu kwa ajili ya watoa huduma wakati wakihudumia watu wenye maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema kuwa mbali na vifaa hiyo shirika hilo limekabidhi zahanati ya kijiji cha Wigelekelo iliyoko kata ya Masela Wilaya ya Maswa, ambayo wameijenga kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho.

“Msaada wote umegharimu kiasi Sh milioni 95,755,000, kwenye zahanati tumetoa pia vifaa mbalimbali vya matibabu, shirika litaendelea kusaidia hasa mapambano dhidi ya COVID -19 na kuhakikisha wananchi wote wanakuwa salama,” amesema Massenza.

Akipokea msaada huo Katibu Tawala Sagini amelishukuru shirika hilo hasa kwa kuwajengea zahanati wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa wakitembea umbali wa kilometa 7 kufuata huduma za afya eneo jingine.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles