25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

World Vision Watoa Vitanda, Magodoro Sekondari Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Shirika lisilokuwa la kiserikali la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vitanda 100 na magodoro 100 katika shule ya sekondari ya Simiyu kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi walioko kambi za kitaaluma kidato cha nne na pili shuleni hapo.

Kupitia mradi wake wa Kanadi shirika hilo limetoa msaada huo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo, kushiriki vyema kambi hizo ambapo awali baadhi yao walishindwa kutokana na kukosa pesa za kununua vifaa hivyo.

Akikabidhi msaada huo leo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo Gilbert Kamanga, Kaimu Meneja wa kanda ya Nzega World vision Gilselda Balyagati alisema kuwa msaada huo umegharimu kiasi cha sh. Milioni 26.6.

Balyagati amesema kuwa World vison imetoa vitana hivyo pamoja na magodoro ili kuunga mkono juhudi za serikali za mtoto kupata elimu bora, ngazi ya shule za msingi na sekondari.

“ Tunatambua kuwa vifaa hivi vitasaidia kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vishawishi na mapambano dhidi ya ndoa na mimba za utotoni, kwani wataweza kuishi shuleni na kuweza kujifunza ipasavyo,” amesema Balyagati.

Naye Ofisa Elimu mkoa Erenest Hinju alishukuru World Vision kwa msaada huo, kwani shule hiyo imeteuliwa kuwa kituo cha kambi za kitaaluma ambapo itapokea wanafunzi wengi kutoka maeneo mengine kwa ajili ya kambi.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga alipongeza shirika hilo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya mkoa katika kuhakikisha sekta ya elimu inafanya vizuri.

Kiswaga alisema kuwa malengo ya mkoa ni kuendelea kushika nafasi za juu kitaifa kwenye mitihani yote ya kitaifa, ambapo aliwataka wanafunzi kutumia vifaa hivyo kuendekea kufanya vizuri zaidi ili kufikia malengo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles