23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WOODS KUREJEA UWANJANI KARIBUNI

CALIFORNIA, MAREKANI

BINGWA wa zamani wa mchezo wa gofu duniani, Tiger Woods, ametangaza kuwa anatarajia kurudi viwanjani hivi karibuni, baada ya kukaa nje kwa miezi nane kutokana na kusumbuliwa mgongo.

Mchezaji huyo amesema ataanza rasmi kushiriki michuano ya ‘Hero World Challenge’, ambayo inatarajia kuanza Novemba 30 hadi Desemba 3, mwaka huu.

Nyota huyo amefanikiwa kutwaa mataji 14 ya kimataifa, lakini miaka mitatu iliyopita alikuwa anasumbuliwa na tatizo la mgongo, hivyo alifanyiwa upasuaji kwa kipindi chote cha miaka mitatu na kuna kipindi alikuwa anafanyiwa upasuaji mara kwa mara, jambo ambalo lilimfanya awe dhaifu.

Alianza kujiondoa kwenye michuano ya Dubai tangu Februari mwaka huu, lakini sasa anaamini afya yake imeanza kukaa sawa, hivyo ana nafasi kubwa ya kuanza kushiriki kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.

“Lengo kubwa kwangu ni kuhakikisha ninarudisha heshima yangu, nitakuwa na furaha kubwa endapo nitafanikiwa kutimiza ndoto hizo, huu ni mchezo ambao ninaupenda katika maisha yangu.

“Mashabiki wangu wakae tayari kuniona uwanjani kabla ya mwaka huu kumalizika, ninaamini afya yangu ipo tayari kushiriki michuano yoyote, hivyo ninaamini nitafanikiwa kurudisha heshima yangu,” alisema Woods.

Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 41, hajafanikiwa kushinda taji lolote kubwa tangu mwaka 2008, hivyo anaamini huu ni wakati wake wa kurudi kwenye ubora kabla ya kustaafu.

“Ni kipindi kirefu sana sijaweza kutwaa taji kubwa la kimataifa, lakini nitakuwa na furaha kubwa endapo safari hii nitakuwa kwenye ubora wangu na kufanikiwa kutwaa baadhi ya mataji kabla ya kustaafu.

“Nadhani sina muda mrefu wa kuendelea kuwa kwenye mchezo huu, hii ni kutokana na umri wangu kuwa mkubwa pamoja na matatizo ninayokumbana nayo katika afya yangu, lakini sijui lini nitastaafu,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles