26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wizkid kutoka na prodyuza Swizz Beatz

Wizkid-Swizz-BeatzLAGOS, NIGERIA

MSANII anayefanya vizuri kwa sasa katika muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, anazidi kupasua anga katika muziki wake baada ya kuweka wazi kuachia wimbo mpya uliorekodiwa na prodyuza wa Marekani, Swizz Beatz.
Mwaka jana prodyuza huyo kupitia akaunti yake ya Instagram, aliwahi kuweka picha ya kava la albamu ya msanii huyo ya ‘Ayo’ hata hivyo aliwahi kuweka video yake ambayo ilikuwa ikimuonyesha akisikiliza wimbo wa msanii huyo wa ‘Ojuelegba’.
Wizkid ameweka wazi kwamba kuna kazi mpya inakuja ambayo amefanywa na prodyuza na wasanii wakubwa duniani.
“Tayari wimbo wangu na Swizz Beatz umekamilika na natarajia kuuachia hivi karibuni, mashabiki wakae tayari kupokea wimbo huo,” aliandika Wizkid.
Hata hivyo, msanii huyo tayari amefanya wimbo na rapa kutoka Young Money, Drake na sasa yupo katika ziara ya muziki na msanii wa RnB, Chris Brown, barani Ulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles