WIZKID, DAVIDO VITA IMEANZA TENA

0
764

LAGOS, NIGERIA


WAKALI wanaofanya vizuri katika muziki nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ na Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, vita yao imeanza tena kwenye mitandao ya kijamii.

Wawili hao wamekuwa kwenye mgogoro kwa kipindi kirefu, lakini miezi michache iliyopita waliweka wazi kumaliza tofauti zao na wakawa wanaonekana wakifanya shoo pamoja, kupiga picha pamoja, lakini mashabiki wamepigwa na butwaa baada ya kuona wasanii hao kila mmoja akimfuta mwenzake kwenye akaunti ya Instagram.

Inadaiwa kwamba Wizkid alikuwa wa kwanza kumfuta Davido, hivyo mashabiki wakawa na maswali mengi ya kujiuliza kwanini msanii huyo amefanya hivyo, hata hivyo Davido aliamua kuwajibu kwa kusema: “Kila mmoja anafanya anachokipenda.”

Hata hivyo, baada ya muda Davido na yeye aliamua kumuondoa Wizkid kwenye akaunti yake. Mashabiki wameonekana kuchoshwa na tabia ya wasanii hao huku wengine wakiwaporomoshea matusi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here