30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara yawafunda watoa huduma za afya

Na Mwandishi Wetu -MWANZA

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imewafunda watoa huduma za afya jijini Mwanza kuhusu utoaji elimu bora kwa kufuata misingi na taratibu za utoaji huduma kwa wagonjwa ili kupunguza maambukizi mapya na vifo visivyo  vya lazima.

Hayo yamelezwa wakati wa semina ya mafunzo kuhusu njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, jijini hapa, ikiwa ni moja ya mikoa iliyoko hatarini kupata ugonjwa wa ebola.

Ofisa Mkuu Uhakiki Ubora kutoka Wizara ya Afya, Dk. Joseph Hokololo, alisema  zaidi ya watu milioni 1.4 duniani wanaugua magonjwa yanayosababishwa na kupata maambukizi mapya wakati wa kupata huduma ya afya, na hii hutokana na watoa huduma za afya kutofuata taratibu za namna ya kutoa huduma.

Alisema asilimia 15 ya wagonjwa hupata maambukizi ya magonjwa mapya katika vituo vya kutolea huduma za afya kutokana na kutofuatwa kwa taratibu, kanuni za miongozo ya kutoa huduma za afya (IPC Guideline, SOP).

Ofisa wa Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya, Dk. Chrisogane Justine, alisema taratibu za utoaji huduma kama kanuni za uoshaji sahihi wa mikono humsaidia mtoa huduma kuzuia kusambaza maambukizi ndani ya kituo cha kutolea huduma.

Licha ya changamoto za upatikanaji wa huduma za majisafi kwa baadhi ya vituo vya afya, Dk. German alisisitiza umuhimu kwa mtoa huduma kuhakikisha ananawa mikono yake vizuri kwa sabuni na majisafi ili kuepuka maambukizi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Akitoa elimu juu ya namna ya kujikinga na maambukizi mapya, Dk. Radenta Bahegwa, alisema asilimia 40 ya magonjwa yanayopatikana katika vituo, yanasababishwa na kutofuata taratibu za miongozo ya utoaji huduma.

Mtaalamu waa Kitengo cha Dharura na Maafa, Dk. Alex Sanga, alisema katika watu 100, watano hadi 10 wanakuwa katika  hali mbaya ya ugonjwa wa kipindupindu, hivyo alitoa wito kwa watoa huduma kuhakikisha wanafuata miongozo.

Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Akili Mwakabhana, alisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo.

Mfamasia kutoka Hospitali ya Kanda ya Bugando, Francisco Chibunda, alitoa wito kwa watoa huduma kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles