24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Uchukuzi yatakiwa kuwajibika

Na Sheila Katikula, Mwanza

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amewataka viongozi wa wizara hiyo kujenga utamaduni wa kukaa na  watumishi wao na kujadili mambo mbalimbali ya utendaji wa  kazi ili kuendeleza uwajibikaji na utekelezaji wa miradi.

Waitara alisema hayo katika hafla ya upokeaji taarifa za utendaji kazi kutoka kwenye taasisi mbalimbali ambapo alisisitiza lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuangalia utekelezaji wa majukumu yao na utendaji wa kazi. 

Alisema ni vema  viongozi kuweka utaratibu wa kuzungumza na watumishi wao ili kuweza  kutambua changamoto zinazowakabili kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza malalamiko kwa wananchi yanayotokana na uwajibikaji hafifu wa baadhi ya watendaji.

Aidha Waitara aliwasisitiza watumishi woye kuendelea kufanya kazi kwa weledi na ubunifu ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ambayo yatasaidia katika utekelezaji wa miradi kwenye maeneo tofauti hapa nchini.

Waitara aliahidi kuwa bega kwa bega na watumishi wa kila taasisi ili waweze  kujadiliana kwa kina juu ya utekelezaji wa majukumu, changamoto, mafanikio na mikakati itakayosaidia Wizara kusonga mbele na kufikia malengo.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya huduma za Meli (MSCL) Philemon Bagambilana alisema wanaendelea na kazi ya uendeshaji wa meli za Serikali katika Ziwa Victoria, ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa kwani lengo ni kuhakikisha huduma ya usafiri wa majini inaboreshwa.

“Ziwa Victoria tuna meli Tisa, Tanganyika tuna meli tatu na boti moja na Ziwa Nyasa tuna meli mbili miongoni mwa meli hizo Kuna ambazo ziko kwenye ukarabati,” amesema Bagambilana.

Naye Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara (Tanroad) Mkoani hapa, Vedastus Maribe alisema kuwa wanaendelea kushirikiana na Wizara kutekeleza miradi mbalimbali iliyopo kwa ufanisi mkubwa ili  kukamilika kwa wakati likiwemo daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 litakalogharimu Sh bilioni 582.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles