22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Nishati yaomba Trilioni 3.04

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nishati, January Makamba ameliomba Bunge kuidhinisha Sh Trilioni 3.04 kwa ajili ya kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Waziri Makamba ametoa hoja hiyo leo Mei 31, 2023 bungeni jijini Dodoma ambapo amesema Sh trilioni 2.96 sawa na asilimia 97.1 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.

“Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Sh 3,048,632,519,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.

“Mchanganuo wa fedha hizi ni kama ifuatavyo: Sh 2,960,702,821,000 sawa na asilimia 97.1 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Sh 2,609,156,128,000 ni fedha za ndani na Sh 351,546,693,000 ni fedha za nje.

“Sh 87,929,698,000 sawa na asilimia 2.9 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Sh 71,637,112,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Sh 16,292,586,000 ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake,” amesema Waziri Makamba.

Aidha, Makamba amesema kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa nishati katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na burudani katika maeneo ya vijijini na vitongojini, wizara itaendelea kuweka mkazo katika kuharakisha upatikanaji wa nishati katika maeneo hayo.

“Tumefanikiwa kuzima mitambo inayotumia mafuta katika Wilaya za Kibondo, Ngara, Kasulu, Biharamulo na Loliondo kwa kuunganisha wilaya hizo na gridi ya taifa. Katika tukio la kihistoria, kwa mara ya kwanza kabisa baada ya miaka mingi tumetimiza ahadi ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa mkoani Kigoma.

”Aidha, katika mwaka ujao wa fedha serikali itaongeza nguvu katika umeme wa gridi ya taifa mkoani Kigoma. Umeme uliopo sasa ni Kilovoti 33, Waziri Makamba amesema sasa serikali inapeleka Kigoma umeme wa Kilovoti 400,” amesema Makamba.

Katika hatua nyingine, Makamba amelihakikishia Bunge kwamba bajeti ya Nishati kwa mwaka 2023/2024 itakamilisha kazi ya ujenzi wa bwawa na kufua umeme la Julius Nyerere linaloendelea kujengwa Rufiji mkoani Pwani.

Waziri Makamba amesema historia itaandikwa ndani ya bajeti hii, kwani mradi huo utaanza kuingiza umeme wake kwenye gridi ya taifa, na kutimiza ndoto iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles